Mjadala wa Wiki

Mkutano wa viongozi wa mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki kuanza leo jumatano, Arusha Tanzania

Sauti 12:26

Viongozi wa mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki wanakutana mjini Arusha hapa Tanzania katika mkutano wa 17 wa jumuia hiyo, EAC.Katika makala hii tunaangazia hatua iliyofikiwa hadi sasa tangu kuundwa kwa jumuia hiyo, ukichukulia kuwa huu ndio mkutano wa kwanza anaosimamia mwenyekiti wa jumuia hiyo na ambaye ndiye rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkta.John Pombe Joseph Magufuli.Pamoja na mambo mengine ikiwemo usalama katika ukanda, maendeleo ya kijamii, na kiuchumi, viongozi hawa wanajadiliana juu ya suala zima la kuikaribisha nchi ya Sudan Kusini,pia Somalia kujiunga na jumuia hiyo pia kuanzishwa kwa hati ya kusafiria, pasipoti kwenye ukanda huo, Njia ya kuzuia mavazi ya mitumba, Kupunguza azma uenezaji wa magari yaliyotumika.Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza makala hii.