UN-BURKINA FASO-USHIRIKIANO

Ban Ki-moon ziarani Burkina Faso

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alifanya ziara yake ya tatu ya kikazi nchini Burkina Faso, Mwanzoni mwa Machi 2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alifanya ziara yake ya tatu ya kikazi nchini Burkina Faso, Mwanzoni mwa Machi 2016. © REUTERS/Denis Balibouse

Ban Ki-moon amewasili Jumatano hii Machi 2 alasiri katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekula chakula cha mchana pamoja na viongozi wa serikali ya Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Kwa ziara hii ya tatu nchini Burkina Faso, Ban Ki-moon amekuja kuwapongeza raia wa Burkina Faso kwa ajili ya mafanikio ya usimamizi wa kipindi cha mpito, ambacho kilimalizika kwa uchaguzi ambao matokeo yake yalikubaliwa na wadau wote.

Ban Ki-moon amekuja mjini Ouagadougou kuwapongeza wananchi wa Burkina Faso na kuonyesha uungwaji wake mkono kwa nchi hii ambayo imekua na hatua muhimu katika historia yake, amesema Ban. "Ninatambua kuwa Burkina Faso inatoka mbali, ilipitia kipindi kigumu tangu tukio la mwezi Oktoba 2014, Ban Amepongeza. Ninapongeza sana ujasiri wa watu wa Burkina Faso. Niko hapa kuwahakikishia ahadi za Umoja wa Mataifa kwenu. "

Roch Marc Christian Kaboré hakumhakikishia Ban Ki-moon tu juu ya utekelezaji wa mchakato unaoendelea nchini Burkina Faso. Lakini pia ametaka msaada wa Umoja wa Mataifa.

"Tarehe 26 Septemba, viongozi wa dunia walipitisha mpango mpya wa maendeleo endelevu kwa miaka 15 ijayo, rais wa Burkina Faso amekumbusha. Nchi yangu ina matumaini kwamba dhamira ya jumuiya ya kimataifa kwa mpango huu mpya wa maendeleo itakuwa changamoto kwa nchi wanachama kuamua zaidi kuandaa malengo ya Milenia kwa kuhakikisha kuwa maendeleo ni njia ya amani na ustawi. "

Ban Ki-moon amesisitiza kuwa familia ya Umoja wa Mataifa itakuwa sambamba na serikali ya Burkina Faso kwa muda mrefu kama serikali hii itakubali kufanya mageuzi yanayotarajiwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatazamiwa kukutana na Rais Kaboré na wanasiasa wengine kadhaa kabla ya kutembelea baadhi ya mafanikio ya kiuchumi na kijamii, kabla ya kuondoka Ouagadougou Alhamisi hii mchana.