BURUNDI-EAC-USHIRIKIANO

Benjamin Mkapa msuluhishi mpya katika mgogoro wa Burundi

Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania.
Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania. © MWANZO MILLINGA / AFP

Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) waliokutana Jumatano katika mkutano wa kilelele nchini Tanzania, wamemteua Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa kama "msuluhishi" katika mgogoro wa Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Benjamin Mkapa atakuwa na kazi ya kufufua mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na upinzani. Nafasi hii imewekwa ili kumsaidia Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ambaye anaendelea rasmi kuwa mpatanishi mkuu katika mgogoro huo.

Tangazo hili lilitolewa na John Magufuli, Rais wa sasa wa Tanzania na mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, wakati wa sherehe rasmi ilioandaliwa mjini Arusha, kaskazini mashariki mwa Tanzania.

"Hii ni habari njema sana kwa sababu itaimarisha timu ya upatanishi katika mgogoro wa Burundi", mwanadiplomasia mmoja wa Afrika, ambaye hakutaka jina lake litajwe amekaribisha uamuzi huo.

"Lakini kwa upande mwengine ni udhalilishaji kwa Rais Museveni." Mazungumzo baina ya Warundi yameshindwa kutokana na kukataa kwa utawala wa Bujumbura kuketi kwenye meza moja na upinzani.

Mazungumzo hayo hayakuendelea kunatokana na ukweli kwamba Museveni alikuwa akijiaandalia uchaguzi wa rais nchini Uganda tarehe 18 Februari, uchaguzi ambao aliibuka mshindi, na hivyo alikuwa hana muda wa kutosha wa kujishughulisha na utatuzi wa mgogoro waBurundi.

Mkapa, mwenye umri wa miaka 77, alikuwa rais wa Tanzania tangu 1995 hadi 2005, wakati ambapo nchi yake ilikuwa ikiwapa hifadhi milioni ya wakimbizi wa Burundi ambao walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita ambavyo vilisababisha maelfu ya raia kupoteza maisha tangu mwaka 1993 hadi 2006. Nchi yake ilituhumiwa wakati huo kuwapa hifadhi waasi wa Kihutu wa Burundi, ikiwa ni pamoja na kundi la waasi la CNDD-FDD, ambalo kwa sasa ni chama kilio madarakani nchini Burundi. Wakati huo waasi hao wa Kihutu walikua vita dhidi ya jeshi lililokua likiongozwa na watu wachache kutoka jamii ya Watutsi.

Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania zimewakilishwa katika mkutano huo wa mjini Arusha na Marais wao. Burundi, ambayo inakumbwa kwa zaidi ya miezi kumi na mgogoro wa kisiasa, uliosababishwa na nia ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu, ambao aliupata mwezi Julai, imewakilishwa na Makamu wake wa pili, Joseph Butore.

Nkurunziza angelichukua nafasi ya rais wa Tanzania kwa kuiongoza Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC). Lakini alikataa tangu awali kushikilia nafasi hii kutokana na mgogoro unaoendelea kuikumba nchi yake "na huenda asipatikani kiurahisi katika mikutano mbalimbali ya Jumuiya hiyo," mwanadiplomasia mmoja amesema.

Muhula wa Rais Magufuli uliongezwa Jumatano hii kwa mwaka mmoja. Pierre Nkurunziza hajaondoka nchini Burundi tangu jaribio la mapinduzi la Mei 13 na 14 mwaka 2015, ambalo lilitokea wakati alipokua katika ziara ya kikazi mjini Dar es Salaam, mji wa kibiashara wa Tanzania, katika mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).