Sudan kusini kuidhinishwa kuwa mwanachama mpya wa jumuia ya afrika mashariki, usalama mashariki mwa DRC

Sauti 20:52
Sayari ya dunia
Sayari ya dunia

Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana katika kikao cha 17 cha marais mjini Arusha Tanzania wiki hii na hivyo kukubaliana kwa pamoja kuwa Sudan Kusini ijiunge rasmi na muungano huo wa Afrika mashariki katika hafla ya kongamano la viongozi wa mataifa wanachama wa EAC.Kujiunga kwa Sudan Kusini kumefikisha idadi ya mataifa wanachama kufikia 6.Mataifa mengine wanachama ni Kenya, Burundi, Rwanda, Tanzania na Uganda.Mbali na hilo, pia katika makala hii tumeangazia hali ilivyo huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na pia barani ulaya.