TANZANIA-SIASA-UTEUZI

William Kijazi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Tanzania

John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015.
John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015. REUTERS/Sadi Said

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amemteua Jumapili hii Mhandisi John William Kijazi kuwa katibu mkuu kiongozi nchini Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Kijazi, Kabla ya kuteuliwa, alikuwa anahudumu kama balozi wa Tanzania nchini India ambapo hivi karibuni alitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha vijana wa Tanzania wanaosomea India wanapata usalama wa kutosha kufuatia shambulizi la hivi karibuni dhidi ya mmoja wao.

Kulingana na taarifa fupi iliotolewa na ikulu ya rais Balozi anaanza kazi mara moja baada ya uteuzi huo.

Bw Kijazi anachukua nafasi iliyowachwa wazi baada ya kuondolewa Balozi Ombeni Sefue.

Taarifa hiyo ya ikulu iliyotiwa sahihi na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa inasema kuwa Sefue atapewa majukumu mengine.