ICC-GBAGBO-BLE GOUDE-SHERIA-HAKI

Kesi ya Gbagbo: Sam Mohamed atoa ushahidi

Chumba cha mahakama wakati kesi ya Laurent Gbagbo ikisikilizwa na ICC, mjini Hague mnamo Januari 28, 2016.
Chumba cha mahakama wakati kesi ya Laurent Gbagbo ikisikilizwa na ICC, mjini Hague mnamo Januari 28, 2016. © REUTERS/Peter Dejong/Poo

Baada ya zaidi ya wiki mbili ya kusimamishwa, kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé inmeendelea Jumatatu hii, Machi 7 kwenye Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire na mshirika wake wa karibu wanahitakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuhusika kwao katika ghasia zilizotokea nchini humo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011.

Wawili ho walikana kosa, na kusema hawana hatia yoyote. Zaidi ya mwezi mmoja baada ya ufunguzi wa kesi hiyo mnamo Januari 28, shughuli za mahakama zinaenda kwa mwendo wa kinyonga. Wiki hii mpya itakua tu ni ya kumsikiliza shahidi watano kutoka upande wa mashtaka kati ya mashahidi 138.

Shahidi wa tano ni Sam Jichi Mohamed, anaejulikana kwa jina la utani Sam Africain. Ni mmoja wa mashahidi wa upande wa mashtaka ambye majina yake yalitolewa kimakosa wakati wa kikao cha pili cha kusikilizwa.

Akivaa kanzu kubwa juu ya Sweat-shirt ya bluu, huku kila kidole kikivikwa pete, mtu, huyo mwenye umri wa miaka 53, aliefika kaskazini mwa Côte d’Ivoire akiwa na umri wa miaka nane, ni raia wa Côte d’Ivoire mwenye asili ya Libanon. Sehemu kubwa ya asubuhi alizungumzia tu maisha yake: ameeleza kwamba ni mfanyabiashara aliyejihusisha katika siasa upande wa Laurent Gbagbo.

Chama cha FPI chaghadhabishwa

"Rais ni baba kwangu," amesema Sam Mohamed Jichi. Wakati wote wa asubuhi, alirejelea suala la kuundwa kwa chama chake, NACIP, moja ya vyama viliomuunga mkono Laurent Gbagbo katika uchaguzi wa mwaka 2010 na ziara alizofanya katika nchi nzima ya Côte d’Ivoire kwa kutetea maridhiano, amesema. Mtu huyu amesema kuwa ni mtu wa amani na ametoa ushahidi ili kujua ukweli, kwa heshima ya wahanga.

Wakati wote wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mwendesha mashitaka alijaribu kuwataja wahusika wakuu wa kampeni ya Laurent Gbagbo au wahusika wa baadhi ya itikadi kupitia Sam L'African ambapo hali hiyo iliibua mjadala mkubwa.

Kama ushahidi wake haupingi urafiki wake kwa Laurent Gbagbo mpaka sasa, chama cha zamani cha rais huyo (FPI) hakikufurahishwa na kufikishwa mahakamani kwa Sam L'Africain. Kutolewa kimakosa cha majina yake kama shahidi wa upande wa mashtaka imesababisha chama chake cha NACIP kutengwa kutoka Muungano wa vyama thelathini unaoongozwa na chama cha FPI cha Pascal Affi N'Guessan.