ICC-GBAGBO-BLE GOUDE-SHERIA-HAKI

Kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude kusikilizwa ICC

Rais wa wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo, siku ya kwanza ya kesi yake Januari 28, 2016.
Rais wa wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo, siku ya kwanza ya kesi yake Januari 28, 2016. © REUTERS/Peter Dejong/Pool

Baada ya zaidi ya wiki mbili ya kusimamishwa, kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé inaendelea Jumatatu hii, Machi 7 kwenye Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire na mshirika wake wa karibu wanahitakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuhusika kwao katika ghasia zilizotokea nchini humo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011.

Wawili ho walikana kosa, na kusema hawana hatia yoyote. Zaidi ya mwezi mmoja baada ya ufunguzi wa kesi hiyo mnamo Januari 28, shughuli za mahakama zinaenda kwa mwendo wa kinyonga. Wiki hii mpya itakua tu ni ya kumsikiliza shahidi watano kutoka upande wa mashtaka.

Angalau siku nne zitakuwa tu za kumsikiliza shahidi huyo watano, ambapo ofisi ya mwendesha mashitaka haitaki kuzungumzo chochote, na haijulikani iwapo shahidi huyo ni mwanamume au mwanamke au pia aina ya uhalifu ambao mtu huyo atatoa ushahidi wake.

Itakumbuka kwamba mbali na hatua za ziri za kawaida, upande wa mashtaka unataka pia kuwa makini zaidi baada ya kurushwa hewani, kwa makosa, majina ya mashahidi wake wanne katika wiki ya pili ya kusikilizwa. Upande wa mashtaka unatarajia kuwasilisha 138, ikiwa ni pamoja na vielelezo 10,000.

Lengo, kama alivyoeleza mwendesha mashtaka katika siku ya kwanza ya kesi: kuonyesha kwamba kwa kutaka kusalia madarakani kwa gharama zote, Laurent Gbagbo alipanga na kuamuru mfululizo wa mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi, mashambulizi ambayo yaliendeshwa na kundi lililoundwana vikosi vya usalama, wanamgambo, mamluki na makundi ya vijana.

Charles Blé Goudé alikua kwenye wa mbele, ambaye alikua akiongoza kundi hili, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka. Kisha, mwakilishi wa wahanga alisisitiza umuhimu wa kuvunja ukimya.

Wanasheria wa upande wa utetezi wa Laurent Gbagbo wameshutumu toleo la upande mwengine katika mgogoro, wakimtuhumu Alassane Ouattara kuwa ulichukua madaraka kwa nguvu, kwa msaada wa Ufaransa. Na Charles Blé Goudé mwenyewe ndiye alihitimisha hotuba ya ufunguzi. "Hakuna tone la damu ninalotuhumiwa kumwaga," alisema Blé Goudé, ambayewa wanasheria wake walimsifu kama mtetezi wa amani.