TUNISIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Tunisia: wapiganaji wa Kiislam wa ziada wauawa Ben Guerdane

Askari wa Tunisia wakipiga doria katika mkoa wa Ben Guerdane, kusini mashariki mwaTunisia, karibu na mpaka wa Libya, Machi 9, 2016.
Askari wa Tunisia wakipiga doria katika mkoa wa Ben Guerdane, kusini mashariki mwaTunisia, karibu na mpaka wa Libya, Machi 9, 2016. REUTERS/Zoubeir Souissi

Jeshi la Tunisia limetangaza kuwa limewaua wanamgambo watatu wa kundi la kigaidi la IS Alhamisi hii wakati wa operesheni ya kijeshi inayoendelea katika mkoa wa Ben Guerdane, kusini mashariki mwa nchi hiyo, karibu na mpaka wa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi la Jumatatu wiki hii dhidi ya mji huo, unaoshambuliwa mara kwa mara na wapiganaji wa kundi la Islamic State, lilizimwa na vikosi vya usalama kwa mapigano ambayo yalisababisha vifo vyazaidi ya watu 50. Mapigano yanaendelea katika eneo hio ambapo jeshi limeendelea kuwakamata wahusika wa shambulizi hilo ambao bado wako hai.

Katika taarifa yake, jeshi limesema kwamba "vitengo vya vikosi vya usalama na jeshi vimewaua magaidi watatu, na vimemkamata mwingine na vimekamata bunduki tano aina ya Kalashnikov Alhamisi hii katika mji wa Ben Guerdane".

Wapiganaji wa Kiislam ambao waliendesha shambulizi Jumatatu wiki hii Alfajiri dhidi ya kambi za jeshi na polisi walikuwa hamsini, kwa mujibu wa serikali.

Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid, amehusisha shambulio hilo kwa wapiganaji wa kundi la Islamic State, linaloendesha harakati zake nchini Libya.