Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Uganda kuwasilishwa mahakamani, Umoja wa ulaya kuiomba DRC kutowabana wapinzani

Sauti 20:47
Sayari ya dunia
Sayari ya dunia

Katika makala hii tumeangazia hatua ya waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi kuwasilisha kesi mahakamani kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi Rais Yoweri Museveni, lakini juma hili mahakama ya Juu ilitoa msimamo wake wa awali wakati kesi ikiendelea.Pia utasikia huko DRC serikali kupitia msemaji wake Lambert Mende iliiomba jumuia ya kimataifa kuisaidia kuboresha swala zima la Haki za binadamu, na Hii baada ya Wajumbe wa Umoja wa Ulaya EU kuishutumu serikali kuwakandamiza wapinzani.Tumeangazia pia mauaji ya Jamhuri ya Afrika ya kati, Uchaguzi nchini CONGO Brazzaville na Mchujo unaoendelea Marekani.Ungana nami Mtangazaji wako Reuben Lukumbuka Ben Saleim.@rlrubenleo, +255686000431.