COTE D'IVOIRE-ETOILE DU SUD-MAUAJI

Côte d'Ivoire: usalama waimarishwa na uchunguzi waendelea

Kwenye ufukwe wa ziwa linalopatikana katika mji wa Grand-Bassam, ambko kulitokea shambulio lililogharibu maisha ya watu 18, Machi 14, 2016.
Kwenye ufukwe wa ziwa linalopatikana katika mji wa Grand-Bassam, ambko kulitokea shambulio lililogharibu maisha ya watu 18, Machi 14, 2016. AFP

Mamlaka ya Cote d'Ivoire imeahidi kuimarisha usalama na kuendeleza uchunguzi wa kwanza kuhusu shambulizi la kijihadi nchini Cot d'Ivoire, shambulizi ambalo liliwaua watu 18 ikiwa ni pamoja na raia wanne kutoka Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lilitokea mwishoni mwa juma lililopita katika mji wa mapumziko wa Grand-Bassam karibu na mji wa Abidjan, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa na ule wa Mambo ya Ndani wanatazamiwa Jumanne kujielekeza.

"Jean-Marc Ayrault na Bernard Cazeneuve watatembelea Jumanne hii mjini Abidjan ili kuonyesha mshikamano wao kwa mamlaka ya Cote d'Ivoir na raia wa nchi hiyo na kuihakikishia uungwaji mkono wao kwa jamii ya Wafaransa waishio katika mji huo," chanzo kilio karibu na Waziri Ayrault, kimebaini.

Katika hotuba iliyorushwa hewani kwenye runinga, Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara amesema "Cote d'Ivoire haitokubali kutishwa na magaidi (...) Hatutaruhusu magaidi kuzorotesha maendeleo yetu ya kuelekea katika ukuaji wa uchumi," Rais Ouattara amesema.

Maeneo yanayotembelewa na wageni wengi tayari yamelengwa na mashambulizi yaliodaiwa kutekelezwa na kundi la AQIM lenye mafungamano na Al Qaeda, katika mji wa Bamako (watu 20 waliuawa ikiwa ni pamoja na wageni14 Novemba 20, 2015) na mjini Ouagadougou (watu 20 waliuawa Januari 15).

Siku chache kabla ya shambulio hilo katika mji wa Ouagadougou, kiongozi wa AQIM kaliwatishia washirika wa nchi za Afrika Magharibi, akimaanisha hasa nchi zinazochangia askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali au nchi ambako wanajeshi wa Ufaransa au marekani wanapiga kambi, kama Cote d'Ivoire na Burkina Faso.

Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cote d'Ivoire Hamed Bakayoko, pia alibaini kuwa mipango ya mashambulizi ilitibuliwa. "Ni kwa miaka kadhaa sasa nchi yetu ikilengwa," alisema waziri Bakayoko.