SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Somalia: Al Shabab yateka baadhi ya maeneo

Gwaride la wapiganaji wapya wa Al Shabab katika mji wa Afgooye, magharibi mwa Mogadishu, Februari 17, 2011.
Gwaride la wapiganaji wapya wa Al Shabab katika mji wa Afgooye, magharibi mwa Mogadishu, Februari 17, 2011. © KENYA-SECURITY/SOMALIA REUTERS/Feisal Omar/Files

Wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia wamedhibiti bandari ndogo ya jimbo la Puntland.

Matangazo ya kibiashara

Gavana wa eneo la Hassan Mohamed, ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa wanamgambo hao wa Al Shabab wakiwa ndani ya maboti wamedhibti bandari hiyo baada ya kuuchukua mji wa Gara'ad .

Shahidi mmoja ambaye hakutaka kutajwa amesema kuwa wapiganaji hao walishusha silaha zao kutoka kwa maboti hayo.

Ripoti zinasema kabla ya kuchukua bandari hii, wanagambo wa Al Shabab walikuwa na kikao na wazee wa eneo hili na kuwaambia kuwa kundi hilo litachukua udhibiti wa maeneo mengi na kuwalenga watu ambao sio Waislamu.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kwamba kundi hilo baadaye liliondoka kwa kutumia barabara baada ya wenzao kuwasili na kuudhibiti mji huo.