DRC-LUCHA-MAANDAMANO

DRC: wanaharakati wa LUCHA wakamatwa

Nje ya mahakama ya Goma, wanaharakati vijana walikusanyika wakiwa na mabango ili kuwaunga mkono ndugu zao "Free Lucha," Februari 22, 2016.
Nje ya mahakama ya Goma, wanaharakati vijana walikusanyika wakiwa na mabango ili kuwaunga mkono ndugu zao "Free Lucha," Februari 22, 2016. © RFI/Sonia Roll

Polisi imewakamatwa Jumanne hii wanaharakati wa shirika la kiraia la LUCHA. Angalau wanaharakati 18 kati yao wamekamatwa wakati wa maandamano yalioendeshwa kwa ukimya katika mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao walikua wakiandamana wakiomba kuachiliwa huru kwa Fred Bauma na Yves Makwambala, wanaharakati wawili wanaozuiliwa jela mjini Kinshasa mwaka mmoja sasa. Wanaharakati hao sasa wameanza mgomo wa kususia chakula usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne hii.

Jumanne hii, wanaharakati ambao kwa mujibu wa waandaaji walikua 45, ishirini kwa mujibu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch, waliandamana kwa ishara ya kutoa wito kwa "kuheshimu uhuru wa kujieleza na kufanya mikutano". Polisi inasema imewakamata wanaharakati 18, lakini shirika la kiraia la LUCHA limesema waliokamatwa ni 19.

"Tuliona magari mawili ya polisi. Waliwakama wanaharakati, wale waliokua wakiwatafuta. Waliwasukuma wanawake. Wote waliokamatwa wamepelekwa kwenye ofisi ya Idara ya Ujasusi. Mpaka sasa hakuna mashitaka yoyote dhidi yao,"ameema Hazina Akili, mwanaharakati wa LUCHA.

Wanaharakati wa LUCHA wanadai kwamba walifanya maandamano kulingana na sheria, baaada ya kutoa taarifa kwa viongozi husika kuhusu maandamano hayo. Madai hayo yanafutiliwa mbali na mkuu wa polisi mjini Goma, Vital Awachango. "Wanahatarisha usalam wa raia. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya mamlaka ya manispa ya jiji ya Desemba 3, hakuna shirika la kiraia la LUCHA ambalo linatambuliwa hapa Goma," Vital Awachango ameelezea.