FIFA-UFISADI

Kashfa ya rushwa: FIFA yawageukia viongozi wa zamani

Gianni Infantino, Rais mpya wa FIFA. Ijumaa Februari 26, 2016 mjini Zurich.
Gianni Infantino, Rais mpya wa FIFA. Ijumaa Februari 26, 2016 mjini Zurich. FIFA TV

Enzi mpya yafunguliwa katika Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA), ambapo rais mpya aliyechaguliwa, Gianni Infantino, ameahidi kurejesha picha na sifa nzuri kwa FIFA kwa kupambana kwa hali na mali dhidi ya rushwa. FIFA imewataka baadhi ya viongozi wa zamani wa shirikisho hilo kujieleza.

Matangazo ya kibiashara

Wiki mbili baada ya uchaguzi wa Gianni Infantino, Shirikisho la Soka Duniani limeanza kubadili mkakati katika kesi inayojulikana kama "Fifagate". Baada ya kulaumiwa na mahakama ya Marekani kwa karibu mwaka mmoja kwa ufisadi mkubwa, Shirikisho la kimataifa la Soka linaonekana kuwa limeathirika kutokana na viongozi walioza kwa rushwa ambao walitumia vibaya nafasi zao kwa kujihusisha na fedha badala ya soka.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano hii, Machi 16, FIFA imetangaza kwamba imeomba fidia kwa watu 41, wengi wao wakiwa maafisa wa zamani wa FIFA, na ambao kwa sasa wanatuhumiwa na mahakama ya Marekani. Kwa hivyo, Shirikisho la Soka Duniani limeomba Mwendesha Mashitaka Mkuu wa jimbo la New York kushughulikia madai yake, kama taasisi iliyofanyiwa unyonge.

Afrika Kusini yashutumiwa kununuwa michuano ya Kombe la Dunia

FIFA inataka sio tu kurejeshewa fedha ziliopitishwa mlango wa nyuma na washitakiwa, lakini pia katika kurejeshewa mishahara, marupurupu na mafao mengine ambayo walilipwa wakati wa shughuli zao katika Shirikisho. FIFA inabaini kwamba fedha hizo zinakadiriwa kufikia mamia angalau ya mamilioni ya Euro, ambapo rais mpya kuzitumia katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Watu wanaolengwa wanatoka katika bara la Amerika. Lakini pia Afrika Kusini, ambayo inashutumiwa kutoa dola milioni kumi kama rushwa ili kuhakikisha inaandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 katika ardhi yake.