WAHAMIAJI-LIBYA-ULAYA-USALAMA

Wahamiaji 129 wakamatwa na walinzi wa pwani ya Libya

Baadhi ya wahamiaji haramu 400 waliokamatwa na mamlaka ya Libya kabla ya kusafirishwa Ulaya, Mei 17, 2015.
Baadhi ya wahamiaji haramu 400 waliokamatwa na mamlaka ya Libya kabla ya kusafirishwa Ulaya, Mei 17, 2015. REUTERS/Hani Amara

Walinzi wa pwani ya Libya wameikamata kwenye pwani ya mji wa Zouara (kilomita 160 magharibimwa mji wa Tripoli) boti iliyokua ikibeba wahamiaji 129 waliokua wakijaribu kuingia Ulaya, wakitokea Libya, msemaji wa kikosi cha wanamaji amesema Jumatano hii.

Matangazo ya kibiashara

"Kitengo cha Walinzi wa pwani kimeikamata boti moja kaskazini-mashariki mwa mji wa Zouara ambapo ilikua ikitokea. Kulikuwa na wahamiaji 129 ndani ya boti hiyo, ikiwa ni pamoja na wanawake kumi," Ayoub Qassem ameliambia shirika la habari la serikali isiyotambuliwa na jumuiya ya kimataifa mjiniTripoli.

"Abiria waliokua ndani ya boti hiyo wamepelekwa katika kituo cha walinzi wa pwani katika mji wa Zouara, na walitakiwa kufikishwa mbele ya mamlaka ya Libya, na Shirika la Msalaba Mwekundu likifahamishwa," Qassem amesema, bila hata hivyo kubainisha ni lini boti hilo lilikamatwa.

Kwa mujibu wa Kanali Qassem, wahamiaji hao ni kutoka Sudan, Misri, Syria, Palestina, Morocco, Ethiopia, Gambia, Nigeria, Senegal na Chad.

Hali hii ya wakimbizi ilianza tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011 baadhi ya watu wakinufaika kwa biashara ya binadamu, na maelfu ya wahamiaji walijaribu kuingia Ulaya kutoka Libya. Pwani ya Italia inapatikana kwenye umbali wa kilomita 300 tu.

Walinzi wa pwani ya Italia wametangaza Jumatao hii kwamba wahamiaji zaidi ya 1,800 wameokolewa tangu Jumanne wiki hii katika pwani ya Libya na miili miwili iliondolewa majini, wakati ambapo shughuli nyingine za uokoaji zilikuwa zikiendelea.

Mwishoni mwa mwezi Januari, wahamiaji zaidi ya 2,500 waliokolewa kwa muda wa siku nne, ikiwa ni pamoja na 1,270 kwa siku moja ya Januari 26.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi (UNHCR), baadhi ya wahamiaji 9,500 waliwasili nchini Italia wakipitia bahari tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakati ambapo zaidi ya 143,000 wamevuka Bahari ya Aegean kati ya Uturuki na Ugiriki.

Kundi la wahamiaji katika mwambao wa Bahari ya Mediterranea kwenye mpaka kati ya Italia na Ufaransa.
Kundi la wahamiaji katika mwambao wa Bahari ya Mediterranea kwenye mpaka kati ya Italia na Ufaransa. REUTERS/Jean-Pierre Amet