AFRIKA KUSINI-FIFA-RUSHWA

Afrika Kusini yakana tuhuma za FIFA dhidi yake

Mashabiki wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) wakiingia mitaani, siku moja kabla ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2010 kwa siku iliyotajwa kama "Vuvuzela day", Jumatano, Juni 9
Mashabiki wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) wakiingia mitaani, siku moja kabla ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2010 kwa siku iliyotajwa kama "Vuvuzela day", Jumatano, Juni 9 Dundas Football Club/CC-Wiki

Baada ya tuhuma za Shirikisho la Soka Dunia (FIFA) dhidi ya Afrika Kusini, Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini amejibu kwa kusema kuwa nchi yake haijatoa rushwa kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2010, ambapo ni michuano ya kwanza kabisa kuchezwa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

"Afrika Kusini hawajatoa rushwa, na wala hawajalishawishi shirikisho la kimataifa la Soka ili kupata kinyume cha sheria ruhusa ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2010," amesema Bw Fikilie Mbalula mbele ya vyombo vya habari.

Katika toleo la kwanza la ripoti yake, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeishutumu Afrika Kusini kwa kuweza kutoa hongo kwa minajili ya kukubaliwa kuandaa michuana ya Kombe la Dunia 2010. Jumatano mchana wiki hii, "ufafanuzi" hata ulitolewa, ukidai kuwa Taasisi ya soka duniani "haikua imeamini" kuwa Afrika Kusini walitoa hongo ili waweze kukubaliwa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia 2010.

Hata hivyo, waziri wa michezo wa Afrika Kusini ametumiya maneno makali dhidi ya FIFA: "Afrika Kusini imeshushiwa hadhi na kuipaka matope kwa yale mazuri iliyoyafanta katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2010, badala ya kupongezwa, inatshutumia kutoa hongo kwa minajili ya maandalizi ya michuano hiyo," amesema Waziri Fikilie Mbalula.

Kulingana na toleo linaloelezwa na Kusini,kitita cha Dola milioni 10 kilitolewa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kkutoka raia wa Afrika waishio katika nchi za Caribbean.operesheni hii ilipitishwa rasmi na FIFA.

Lakini kama rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Amerika ya Kaskazini na Caribbean (CONCACAF) Jack Warner alichukua fedha hizo kinyume cha sheria, Afrika Kusini haipaswi kulaumiwa kwa hilo, waziri ameeleza.

"Kashfa ya FIFA ya (...) ya husiano haramu kati ya Afrika Kusini na (Jack) Warner ni ni jambo la kupuuziwa," amesema Waziri.

Fifa ilikumbwa na mfululizo wa kashfa za rushwa ambao zilipelekea kujiuzulu na kusimamishwa kwa rais wa zamani Sepp Blatter lakini pia ya viongozi wengine wengi wa taasisi hiyo ya kimataifa.