NIGER-MASHAMBULIZI-USALAMA

Mashambulizi mawili ya kigaidi Niger

Capture d'écran d'une vidéo de propagande de Boko Haram montrant son chef Abubakar Shekau, le 20 janvier 2015. Dans la vidéo diffusée le 1er avril, le chef terroriste n'apparaît pas.
Capture d'écran d'une vidéo de propagande de Boko Haram montrant son chef Abubakar Shekau, le 20 janvier 2015. Dans la vidéo diffusée le 1er avril, le chef terroriste n'apparaît pas. © AFP PHOTO / BOKO HARAM

Nchini Niger wakati zikisalia siku tatu kabla ya uchaguzi wa urais hali ya usalama imeendelea kudorora ambapo vikosi vya usalama na ulinzi vimekua vikilengwa.

Matangazo ya kibiashara

Askari polisi watatu waliuawa Alhamisi Machi 17 katika shambulizi lililohusishwakundi la AQMI lenye uhusiano na al-Qaeda kusini magharibi mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Burkina Faso, wakati ambapo askari mmoja aliuawa katika shambulio la kujitoa mhanga lililohusishwa kundi la Boko Haram, katika mji wa Bosso, katika jimbo la Diffa kusini mashariki mwa nchi, Waziri wa Mambo ya ndani wa Niger Hassoumi Massaoudouameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Mashambulizi yote haya yanatokea ikiwa zinasalia tu siku zisiozidi tatu ili kufanyike duru ya pili ya uchaguzi Jumapili Machi 20, uchaguzi ambapo utampelekea rais anaye maliza muda wake, Mahamadou Issoufou, kusalia madarakani.

Washambulizi watano wa kujitoa mhangamhanga, vijana wawili na wavulana watatu, waliingia katika mji wa Bosso nchini Nigeria, viongozi wa mji huo wamebaini. Wote wameuawa kwa kupigwa risasi, lakini askari watatu wa Nigeria walishambuliwa kwa vipande vya bomu. Mmoja wao, mkuu wa eneo la Bosso, amefariki kutokana na majeraha.

Halmashauri ya mji wa Diffa imeeleza kwamba mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua wakati ambapo mwanajeshi mmoja alikua akichunguza mwili wake ili kuhakikisha hakuna majeraha aliyoyapata. Boko Haram inatekeleza mara nyingi mashambulizi yake kwakutokea nchini Nigeria kwenye mpaka karibu na Ziwa Chad.

Katika shambulio jingine, kusini magharibi mwa nchi, katika mji wa Dolbel, katika mkoa wa Tera, wauaji waliwaua askari watatu katika kituo kilio karibu na mpaka na Burkina Faso. Kwa mujibu wa viongozi wa eneo hilo, shambulio ilo liliendeshwa na watu waliokua kwenye pikipiki na gari ndogo (4X4) muda mfupi kabla ya usiku wa manane Jumatano Machi 16. baada ya shambulio hilo wauaji hao waliondoka pamoja na silaha za polisi waliouawa na watu wao waliojeruhiwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Hassoumi Massaoudou amesema kuwa shambulizi hilo limeendeshwa na kundi la AQIM, bila kutoa maelezo zaidi. Kundi la al-mourabitoune linaloongozwa na Moktar Belmokthar, ambalo limerejea AQMI, linaendelea na mashambulizi kwenye eneo la mpaka kati ya Mali, Burkina Faso na Niger.