CONGO-UCHAGUZI-SIASA

Congo-Brazzaville: matokeo ya duru ya kwanza yasubiriwa

Wapiga kura kujipanga katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa rais katika mji wa Brazzaville, Machi 20, 2016.
Wapiga kura kujipanga katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa rais katika mji wa Brazzaville, Machi 20, 2016. © REUTERS/Roch Bouka

Nchini Congo-Brazzaville, wapiga kura walitakiwa kupiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais. Rais anayemaliza muda wake Denis Sassou-Nguesso, madarakani kwa miaka 32 sasa, anakabiliwa na wagombea wanane.

Matangazo ya kibiashara

Tangu usiku wa manane siku ya Jumamosi hadi Jumatatu mawasiliano yamekatika: hakuna ujumbe wa simu, hakuna mawasiliano ya simu kwa sababu za usalama kwa mujibu wa mamlaka. Katika kituo cha kupigia kura cha Angola-huru, zoezi la kuhesabu lilifanyika katika ulinzi mkali. Polisi ilitawanya watu 200 karibu na kituo cha kupigia kura.

Katika kituo hicho, watu mia moja walikuwa wamekusanyika ili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri, katika mazingira mazuri, baadhi ya watu wamekua wakiangalia kuptia dirisha kituo hicho cha kupigia kura, wakiwa wameshikilia kalamu mkononi, ili kujifanyia mahesabu wenyewe.

Kulikuwa na wawakilishi wa wagombea mbalimbali hata kama wote hakuwatuma wajumbe wao. Vikosi vya usalama vilitoa ulinzi mkali, baada ya kutumwa kwa wingi katika mji wa Brazzaville kwa ajili ya kuthibitisha kwamba magari yaliopewa vibali yanatembelea maeneo yote. Mvutano uliibuka Jumapili jioni.

Polisi wa kutuliza ghasia wa Congo iliwatawanya kwa mabomu ya machozi kiasi cha watu 200 waliokusanyika katika kituo cha kupigia kura cha kusini mwa mji wa Brazzaville. Watu hao walikua wakisisitiza lili waweze kuingia kuhudhuria kwa karibu zoezi la kuhesabu kura. Karibu 18:30 jioni (saa za Congo), Askari polisi wengi wenye silaha za kivita walirusha mabomu ya machozi na kuwafukuza kwa muda mfupi vijana hao wafuasi wa mgombea wa upinzani Guy Brice Parfait Kolélas, ambao walikua wakiimba nyimbo za kumsifu kiongozi wao hadi walipoondoka eneo hilo.

Kwa sasa, hali ni shwari. Magari ya kivita na mizinga ya kurusha maji yamepiga kambi katika maeneo mbalimbali.