BENIN-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Benin: Lionel Zinsou akubali kushindwa

Bango la kampeni la Patrice Talon, katika mkoa wa Cotonou.
Bango la kampeni la Patrice Talon, katika mkoa wa Cotonou. © REUTERS

Wakati ambapo matokeo rasmi ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Benin bado hayajatangazwa, katika usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Lionel Zinsou, amekubali kuwa ameshindwa na kumpongeza mfanyabiashara Patrice Talon kwa ushindi wake.

Matangazo ya kibiashara

"Matokeo ya awali yanaonyesha ushindi wa wazi wa Patrice Talon," Lionel Sinzou amesema kwa njia ya simu usiku akiliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP, akiongeza kuwa "kiwango cha ushindani ni kikubwa."

"Nimemuita Patrice Talon usiku wa kuamkia leo ili kumpongeza kwa ushindi wake, na kumtaika mafanikio mazuri na kumniweka karibu yake kwa ajili ya maandalizi ya masuala ya mpito. Nilikuwa na mazungumzo mazuri pamoja naye," amesema Waziri Mkuu anayemaliza muda wake.

Matokeo rasmi ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais hayajajulikana, lakini mfanyabiashara Patrice Talon atakuwa rais mtarajiwa wa Benin. Atamrithi Thomas Boni Yayi. Madarakani tangu mwaka 2006, kwa mujibu wa Katiba inayoruhusu mihula miwili, hakuwa mgombea katika uchaguzi huu.

AFP inaarifu pia kuwa Lionel Zinsou amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENA) inaweza kutangaza matokeo ya awali "pengine katika siku ya Jumatatu."

Uchaguzi bila ya tukio lolote

Jumapili hii, zoezi la kupiga kura lilifanyika kwa amani. Baadhi ya wapiga kura milioni 4.7 walipiga kura katika vituo vya kupigia kura 7908 nchini humo. Mratibu wa shirikisho la mashirika la kiraia pia amekaribisha zoezi hilo lilivyofanyika kwa amani. ameuzungumzia uchaguzi huo kama "siku kuu nzuri ya uchaguzi" huku akisikitishwa kutokana na majaribio ya kujaza kura zisio halali katika masanduku ya kura katika maeneo kadhaa.

Wakati wa duru ya pili, tuliona kuwa msongamano haukua wa kusisimua kama katika duru ya kwanza lakini wale wote ambao walihamasishwa, kwa kweli waliweza kupiga kura kwa uhuru, bila shinikizo: "Hii ni bahati hapa, tunajua kama hali kama hii haitikei katika nchi nyingi za Afrika. Tunaridhika na demokrasia yetu," amesema mpiga kura mmoja.