CONGO-UCHAGUZI-SIASA

Congo: Sassou-Nguesso achaguliwa rais katika duru ya kwanza

Rais Denis Sassou-Nguesso yuko mamlakani kwa kipindi cha miaka 32 katika nchini Congo-Brazzaville.
Rais Denis Sassou-Nguesso yuko mamlakani kwa kipindi cha miaka 32 katika nchini Congo-Brazzaville. © Wikimedia

Kulingana na matokeo rasmi, Rais anayemaliza muda wake Denis Sassou-Nguesso amepata ushindi katika uchaguzi wa rais wa Machi 20, katika raundi ya kwanza kwa 60.39% ya kura, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo-Brazzaville, Raymond Mboulou Zéphyrin, amesema.

Matangazo ya kibiashara

Guy Brice Parfait Kolélas anachukua nafasi ya pili, akifuatiwa na jenerali Jean-Marie Michel Mokoko.

Imethibitishwa tayari. Rais anayemaliza muda wake Denis Sassou-Nguesso amechaguliwa tena katika duru ya kwanza kwa 60.39% ya kura. Waziri wa Mambo ya Ndani Raymond Mboulou Zéphyrin, ametangaza matokeo ya uchaguzi wa rais twa arehe 20 Machi katika runinga ya taifa ya Congo usiku wa manane wa Alhamisi hii.

Guy Brice Parfait Kolélas anachukua nafasi ya pili kwa 15.05%, akifuatiwa na jenerali Jean-Marie Michel Mokoko ambaye amepata 13.89% ya kura. Matokeo ya wagombea wengine sita walioshiriki katika uchaguzi huo hayajajulikana bado.

Jumatano, wagombea wote wawili walipinga matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyotangazwa siku moja kabla na Tume huriu ya Kitaifa ya Uchaguzi (CNEI), ambayo ilimtangaza rais anaye maliza muda wake kuwa ameshinda uchaguzi huo kwa alama 67% ya kura.

Jumapili, zoezi la kupiga kura lilifanyika bila kuwepo na mawasiliano ya simu nchi kote, kwa sababu ya "usalama wa umma", Mamlaka ya Congo ilisema.

Denis Sassou-Nguesso, mwenye umri wa miaka 72, anashikia madaraka kwa kipindi cha miaka 32 nchini Congo-Brazzaville. Kuwania kwake katika uchaguzi huo kuliwezekana kufuatia marekebisho ya Katiba mwishoni mwa mwaka 2015, kwani baadhi ya vipengele vya Katiba hiyo vilikua havimruhusu kugombea kwa mara nyingine tena. Hata hivyo upinzani ulilaani kitendo hicho cha kuifanyia marekebisho Katiba ukisema kuwa ni "mapinduzi ya kikatiba".