DRC-UN-MONUSCO

DRC yaitaka UN kupunguza askari wake

Askari walinda amani wa Monusco,Oktoba 23, 2014 Béni, mashariki mwa DRC.
Askari walinda amani wa Monusco,Oktoba 23, 2014 Béni, mashariki mwa DRC. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inataka Umoja wa Mataifa kupunguza idadi ya wanajeshi wa MONUSCO nchini humo kufikia mwisho wa mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakuja wakati ambapo muda wa kuhudumu kwa askari wa MONUSCO 20,000 ukitarajiwa kumalizika mwezi huu.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa unasema unapanga kupunguza wanajeshi 1,700 tu kwa sababu za kiusalama.

Waziri wa Mambo ya nje wa Congo, Raymond Tshibanda, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, tayari wameshaanza mazungumzo na viongozi wa MONUSCO kuhusu kuondoka kwa wanajeshi hao.

Aidha, Waziri Tshibanda amesema tayari serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza mikakati ya kuwatuma wanajeshi wa FARDC hasa Mashariki mwa nchi hiyo kuanza kukabiliana na makundi ya waasi yanayohatarisha usalama wa raia hasa katika maeneo mabalimbali ya mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Marekani kupitia Balozi wake katika Umoja wa Mataifa Samantha Power, imesema haiungi mkono pendekezo la serikali ya DRC kwa sababu za kiusalama.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon naye amesema anahofia kudorora kwa usalama wakati nchi hiyo ikielekea uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.