MALI-COTE D'IVOIRE-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Mali: watu wawili wakamatwa kwa tuhuma za mashambulizi ya kigaidi

Jeshi la Mali katika eneo la kaskazini, mjini Goundam, karibu na mji wa Timbuktu, mwezi Juni mwaka 2015.
Jeshi la Mali katika eneo la kaskazini, mjini Goundam, karibu na mji wa Timbuktu, mwezi Juni mwaka 2015. © AFP/PHILIPPE DESMAZES

Nchini Mali, watuhumiwa wawili muhimu walikamatwa Ijumaa na Jumamosi hii, 26 Machi katika operesheni mbili tofauti kaskazini mwa Mali, katika uhusiano na mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi ya mjini Grand-Bassam, nchini Côte d’Ivoire, wiki mbili zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Mtu anayejulikana kwa jina la Ibrahim Ould Mohamed alikamatwa kaskazini magharibi, karibu na mji wa Timbuktu, wakati ambapo Mydi Ag Sodack Diko alikamatwa kusini mwa mji wa Gao.

Kwa mujibu wa wachunguzi, watu hao wawili ambao wamesafirishwa mjini Bamako, wanahusishwa katika mashambulizi ya Machi 13 dhidi ya mji wa mapumziko wa Grand-Bassam, nchini Cote d'Ivoire.

Mtuhumiwa wa kwanza, Mydi Ag Sodack Diko, alikamatwa siku ya Jumamosi, kusini mwa mji wa Gao, katika kijiji cha Gossi. Raia huyo wa Mali, kwa mujibu wa ripoti ya kwanza ya uchunguzi, "alishiriki kikamilifu katika mashambulizi ya ya mjini Grand Bassam" nchini Côte d’Ivoire, hasa akihifadhi vifaa viliotumiwa katika shambulizi hilo. Nyumba yake ilioko mjini Abidjan, pia ilitumiwa kwa kuwahifadhi washambuliaji, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa operesheni hiyo. Muda mfupi baada ya shambulio hilo, mtuhumiwa anadaiwa kuwa aliondoka kutoka mji wa Abidjan, kwenda Bamako, kabla ya kuelekea kaskazini mwa Mali ambako alikamatwa.

Mtiuhumiwa wa pili alikamatwa kilomita 80 na mji wa Timbuktu, hasa katika kijiji cha Goundam, katika usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi. Ibrahim Ould Mohamed pia ni raia wa Mali. Kwa mujibu wa mmoa wa wapelelezi, Ibrahim Ould Mohamed alitoa taarifa muhimu na simu yake, ambayo namba yake ni rahisi kukumbuka, alitoa ushahidi wa kutosha. Kama mtuhumiwa wa kwanza aliekamatwa, ni mshirika wa karibu na hata dereva wa Kunta Dallah yalieonyeshwa na vikosi vya usalam vya Côte d’Ivoire, kama kiongozi wa mashambulizi ya Machi 13 ambayo yalisababisha vifo vya watu 19 na thelathini waliojeruhiwa, katika mji wa Grand -Bassam. Mapema siku ya Jumapili mchana, watu hao wawili waliokamatwa walikua katika utaratibu wa kusafurishwa katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

Kama sehemu ya uchunguzi wa mashambuliziya mjini Grand-Bassam, watu kumi na tano wameikamatwa, wakati ambapo mtuhumiwa mkuu, Kunta Dallah, bado hajakamatwa. Mjini Bamako au Abidjan, wanaamini kwamba mtuhumiwa huyo mkuu atakamatwa kutokana na ushirikiano kati ya vyombo vya usalama vya nchi zote mbili.

Kundi la AQMi lenye mafungamano na Al-Qaeda lilikiri kuhusika katika mashambulizi ya mjini Grand-Bassam. Kaskazini mwa Mali, maeneo ambayo bado zaidi yameshindikana kudhibitiwa na majeshi ya Mali na yale ya kigeni, yanaendelewa kukaliwa na makundi yenye uhusiano na AQMI.