CAR-SIASA-USALAMA

CAR: Rais Touadéra achukua hatamu ya uongozi wa nchi

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra, Februari 12, 2016, Bangui.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra, Februari 12, 2016, Bangui. REUTERS/Siegfried Modola/Files

Rais wa kwanza wa Jamhuri ya 6 nchini Jamhuri ya Afrika Faustin-Archange Touadéra, aliechaguliwa Februari 14, 2016, ametawazwa Jumatano hii mjini Bangui.

Matangazo ya kibiashara

Rais Touadéra atakua na kazi kubwa hasa ya kuweka sawa nchi hiyo iliogawanyika katika kipindi cha miaka mitatu ya machafuko ya kijamii.

Marais na viongozi kadhaa wa serikali kutoka nchi za kigeni, au wawakilishi wao kutoka barani Afrika na wajumbe wakuu kutoka kwa wafadhili wa nchi hiyo (Umoja wa Mataifa, Ufaransa, ...) wamehudhuria sherehe ya kuapishwa kwake ambayo inaashiria mwisho wa kipindi cha mpito kilichotokana na kutimuliwa madarakani kwa Rais wa zamani François Bozizé mwaka 2013. Bozize alitimuliwa madarakani na kundi la waasi lenye waislamu wengi la Seleka lililokua likiongozwa na Michel Djotodia.

Tangu wakati huo nchi hii ilitumbukia katika mzunguko wa mauaji ya kijamii na ya kidini, katika historia yake, na kusababisha kuingilia kati kwa majeshi ya kigeni, hususan majeshi ya Ufaransa, wakoloni wa zamani wa nchi hiyo, na kupelekwa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa.

Baada ya kufukuzwa madarakani kwa kutokua na uwezo wa kukomesha mauaji, Bw Djotodia alirejelewa kwenye nafasi yake na Catherine Samba-Panza, ambaye usimamizi wake ulikosoa kwa kipindi cha miezi kadhaa.

Hata hivyo, kipindi cha mpito bado hakijakamilika rasmi. Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliidhinisha kwa kura ya maoni Katiba ya Jamhuri ya 6 na kumchagua rais wao, lakini Bunge bado halijawekwa. Duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge, ambayo iliahirishwa mara kadhaa, sasa imepangwa kufanyika Alhamisi wiki hii, siku moja baada ya kuapishwa kwa rais wa nchi hiyo.