CONGO-UCHAGUZI-SIASA

Congo-Brazzaville: upinzani wawataka raia kusalia nyumbani

Mkutano wa kampeni ya jenerali Mokoko katika mji wa Brazzaville, Machi 18, 2016.
Mkutano wa kampeni ya jenerali Mokoko katika mji wa Brazzaville, Machi 18, 2016. © Manu Pochez / RFI

Nchini Congo-Brazzaville, wagombea wanne waliokata tamaa na uchaguzi wa rais wametoa wito kwa operesheni ya "kususia kazi", Jumanne, Machi 29, katika mji wa Brazzaville na katika nchi nzima.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ina lengo la kupinga ushindi wa duru ya kwanza, wa Rais Denis Sassou Nguesso katika uchaguzi uliofanyika Machi 20.

Katika mji wa Brazzaville, upinzani umewatolea wito wakazi wa mji huo kusalia makwao ili kupinga dhidi ya kile kinachoonekana kama "ujanja wa uchaguzi." Claudine Munari, Kiongozi wa chama cha MUST, ni moja ya vyama viliotia saini kwenye waraka unaotolewa wito raia kususia kazi.

"Hatua hii ni ya kwanza.Tutatekeleza vitendo vingine. Wakati huu, ni "kususia kazi" kila mtu atabaki nyumbani kwake. Hii ina maana kwamba hakuna mtu atakaekwenda ofisini, hakuna mtu atakaefanya kazi. Kwa vyovyote vile, watu wengi watasaila nyumbani. Tutatathmini matokeo ya siku hii ya "kususia kazi" na tutaendelea na vitendo ili kufikia kuonyesha matokeo ya kweli ya uchaguzi wa rais, " Claudine Munari ameiambia RFI.

Kwa upande wake, chama madarakani nchini Cono-Brazzaville kinalaani dhidi ya operesheni hiyo ya "kususia kazi". Akihojiwa na RFI, Pierre Ngolo, katibu mkuu wa chama tawala cha Labour Party, amebaini kwamba upinzani unaweza kuwasilisha malalamiko yake katika mahakama ya Katiba na kusubiri iwapo mahakam hii itatoa uamuzi juu ya uhalali wa matokeo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, upinzani una siku kumi na tano baada ya tangazo la matokeo ya uchaguzi, hii ni kusema kuwa hadi Aprili 7, kuwa wamekata kukata rufaa.