SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Sudan Kusini: kundi la kwanza la waasi wa Riek Machar lawasili Juba

Kundi la kwanza la askari waasi wa Sudan Kusini waliwasili Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa miezi saba iliyopita kati ya makundi hasimu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini kwa zaidi ya miaka miwili, kundi la waangalizi wa kimataifa limetangaza.

Askari thelathini na tisa waasi wamewasili mjini Juba kwa jumla ya 1.370 wanonatarajiwa kama sehemu ya mkataba wa amani ulioafikiwa mwezi Agosti mwaka 2015, Tume ya ufuatiliaji na tathmini ya makubaliano (JMEC) imebaini. Tume hii iliundwa na jumuiya ya kikada ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

Waangalizi wa kimataifa pia wamemtolea wito kiongozi wa waasi Riek Machar kushikilia nafasi ya Makamu wa Rais.

"Hakuna tena vikwazo kwa Makamu wa Rais alieteuliwa kurudi na uundwaji wa serikali mpya ya mpito ya umoja wa kitaifa," Festus Mogae, ambaye anaongoza JMEC, amesema.

Riek Machar aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais Februari 12 na hasimu wake Rais Salva Kiir, ikiwa inaonekana kama ishara ya maendeleo katika utekelezaji wa mkataba wa amani. Lakini mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja na ya mpito badoumekwama, na mapigano yanaendelea katika nchini changa duniani.

Sudan Kusini ilitangaza uhuru wake mwezi Julai 2011, baada ya miongo kadhaa ya mgogoro na Khartoum, kabla ya kutumbukia tena miaka miwili na nusu baadaye katika vita kwa sababu ya kugawanyika kutokana na sababu za kisiasa na kikabila ndani ya jeshi, sababu zilizochochewa na uhasama kati ya Salva Kiir na Riek Machar.

Hayo yakijri, Umoja wa Mataifa, Jumanne hii, umeonya kuwa njaai mefikiwa katika kiwango cha "kutisha" nchini Sudan Kusini, ambapo bei za vyakula ni kubwa mno baada ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliokumbwa na mauaji na tuhuma za uhalifu wa kivita.

"Ripoti ya kutisha ya njaa, utapiamlo na viwango vya janga la uhaba wa chakula vimeshuhudiwa katika maeneo mengi yaliokumbwa na machafuko," shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kilimo ( FAO) limesema katika taarifa yake.