UGANDA-BESIGYE-SIASA-USALAMA

Besigye: “sintotumia nguvu kwa kuindoa NRM madarakani”

Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye.
Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye. © AFP PHOTO / ISAAC KASAMANI

Nchini Uganda, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha upinzani cha FDC Kizza Besigye amesema hatatumia nguvu katika harakati za kuindoa serikali ya NRM madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Besigye wamekuwa wakimtaka kiongozi wao kutumia nguvu lakini Besigye anasisitiza kuwa mbinu iliyotumiwa na rais Yoweri Museveni mwaka 1986 ya vita vya msituni sio sahihi kwa sasa.

Besigye amewaambia wafuasi wake na wanaharakati nyumbani kwake Kasangati anakozuiliwa kuwa ushindi wake ulipokonywa na kuongeza kuwa itawachukua muda kupata haki.

Kwa zaidi ya siku 40 sasa Besigye amekuwa akizuiliwa na polisi nyumbani kwake, Kasangati.