COTE D'IVOIRE-MAKABIKIANO-MAUAJI-BOUNA

Côte d’Ivoire: hali ya utulivu yarejea Bouna

Mfugaji wa ng'ombe, Côte d'Ivoire.
Mfugaji wa ng'ombe, Côte d'Ivoire. © Getty Images/Eco Images

Hali ya utulivu imeanza kushuhudiwa katika mji wa Bouna nchini Cote Dvoire ulio mpakani na Burkina Faso pamoja na Ghana, ambako tangu mapama mwezi huu kukiripotiwa vitendo vya ulipizaji kisasi baina ya wakulima na wafugaji wa makabila ya wa Malinkee na Kulango.

Matangazo ya kibiashara

Wakulima wamekuwa wakiwahutumu wafugaji kuharibu mimea yao kwa kulishiza mifugo yao.

Watu 25 walipoteza maisha katika machafuko hayo akiwemo afisa mmoja wa polisi huku watu wengine zaidi ya 40 wakijeruhiwa.

Vikosi vya usalama kwa ushirikiano na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa nchini humo pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali wameelekea katika eneo hilo ili kuwahamasisha raia kuishi kwa amani.

Ma mia ya watu walitoroka makwao kufuatia machafuko hayo na kukimbilia ncihini Burkina Faso.