DRC-UPINZANI-KATUMBI-SIASA

DRC: Moïse Katumbi atawazwa kuwa "mgombea wa urais"

Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga Moïse Katumbi katika mahojiano mjini Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga Moïse Katumbi katika mahojiano mjini Lubumbashi, Juni 2, 2015. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kamati kuu ya muungano wa vyama 7 vya upinzani G7 imemteua rasmi Jumatano hii mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga, Moïse Katumbi kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya muungano huo.

Matangazo ya kibiashara

Vyama hivi vilioondolewa hivi karibuni katika muungano unaounga mkono chama tawala cha PPRD.

Bila ubishi wowote, Moïse Katumbi ameteuliwa rasmi kuwa mgombea wa G7 katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tangazo hili limetolewa Jumatano Machi 30 baada ya mkutano wa kamati kuu ya muungano unaojumuisha vya saba vya upinzani vilioondolea serikalini, uliofanyika mjini Kinshasa. Vyama hivi viliondolewa katika muungano wa vyama vinavyokiunga mkono chama tawala cha PPRD, baada ya kuonyesha msimamo wao wa kupinga muhula wa tatu wa rais Joseph Kabila.

G7 imemuomba Moïse Katumbi kushiriki uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika Novemba 27.

Siku moja kabla ya uteuzi huo, mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga alikua amesha jiandaa kuwania katika kinyang'anyiro hicho, ambapo alikemea vikali mjini Lubumbashi, kusini mwa nchi hiyo "uchaguzi wa Wakuu wa Mikoa" ambao aliutaja kuwa "uligubikwa na kasoro nyingi".

Hata hivyo Katika mkoa huo mpya wa Katanga, muungano wa vyama vilio serikalini vilipata ushindi katika uchaguzi wa wakuu wa Mikoa uliofanyika Machi 26, huku wagombe wa muungano wa G7 wakibatilishwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kwa "ombi la moja kwa moja" la muungano wa vyama vilio serikalini, jambo ambalo Moïse Katumbi, alikemea pia, akibaini kwamba hiyo ni moja ya dalili zinazoonyesha "jinsi gani sheria zinadidimizwa na demokrasia kotoendelea nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo".