MISRI-USAFIRI-UTEKAJI NYARA

Misri: “utekaji nyara wa ndege ya EgyptAir si tukio la kigaidi”

Ndege ya shirika la ndege la Misri EgyptAir.
Ndege ya shirika la ndege la Misri EgyptAir. PASCAL PAVANI /AFP

Imebainika kuwa mtekaji nyara raia wa Misri aliyolazimisha ndege ya abiria kutua nchinu Cyprus hakuwa na vilipuzi kama alivyodai wakati wa utekaji nyara huo.

Matangazo ya kibiashara

Misri na Cyprus zinasema, tukio hilo lililotekelezwa na Seif Eldin Mustafa halikuwa la kigaidi.

Mustafa anasema wakati wa utekaji nyara huo alikuwa anasumbuliwa kisaikolojia.

Mtekaji nyara huyo miongoni mwa madai aliyotoa ni kutaka kuonana na mke wake zamani ambaye aliletwa katika uwanja wa ndege.

Abiria wote na wafanyika wa Shirika la Ndege la Misri wamerejea nyumbani salama.