UN-DRC-MONUSCO-USHIRIKINAO

UN yajiandaa kurejelea upya muda wa MONUSCO DRC

Askari wa MONUSCO,Okotoba 23, 2014, Beni.
Askari wa MONUSCO,Okotoba 23, 2014, Beni. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano, Machi 30, linatazamiwa kurejelea upya muda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo (MONUSCO) kuendelea na majukumu yake nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kinyume na mapendekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ya Desemba 2015, Umoja wa Mataifa unapania kupunguza idadi ya wanajeshi wake kama hali ya usalama itakaua imeboreka.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litatia kipao mbele hasa kwa ushirikiano kati ya MONUSCO na majeshi ya DR Congo (FARDC) mashariki mwa nchi hiyo kwa kupambana dhidi ya makundi ya waasi. Ulinzi wa raia ni utapewa kipao mbele, wakati ambapo visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vimeendelea kuongezeka katika kipindi hiki cha kabla ya uchaguzi.

Kurejelea upya muda wa MONUSCO nchini DR Congo imekua ni shughuli ya mvutano wa kila mwaka kati ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya Kishasa, ambayo inataka Ujumbe huo uondoke nchini humo. Ni miaka 16 sasa Ujumbe wa MONUSCO ukiendesha shughuli zake nchini DR Congo, hasa mashariki mwa nchi hiyo.

Lakini mwaka huu, kura hii ambayo itafanyika Jumatano hii Machi 30, inafanyika katika mazingira ya kipekee pamoja na muhula wa mwisho wa Joseph Kabila na hofu ya kumuona akiendelea kusalia madarakani na kusababisha mgogoro mpya wa kikatiba katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Hakuna suala la kupunguza idadi ya askari 1700 wa MONUSCO, kama ilivyopendekezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Desemba mwaka jana.