LIBYA-USALAMA-SIASA

Libya: Tripoli katika hali ya taharuki baada ya kuwasili Waziri Mkuu

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Machi 30, 2016.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Machi 30, 2016. AFP

Nchini Libya, Waziri Mkuu aliyeteuliwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa hatimaye aliwasili Jumatano Machi 30 katika mji wa Tripoli.

Matangazo ya kibiashara

Kuwasili kwa Fayez el-Sarraj kumesababisaha kuzorota kwa hali ya usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo. Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya, Marekani, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa wamekaribisha ujio wa Waziri Mkuu wa Libya katika mji wa Tripoli.

Hata hivyo serikali hiyo inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, inapingwa na serikali mbili sambamba, zisiotambuliwa na jumuiya hiyo: serikali moja ina makao yake makuu katika mji wa Tripoli na nyingine katika mji wa Tobruk. Hali ya mvutano ilijitikeza Jumatano jioni kati ya wanamgambo baada ya kuwasili kwa kiongozi huyo mjini Tripoli kwa njia ya bahari.

Kulisikika milio ya risasi katika maeneo mbali mbali ya mji mkuu wa Libya, Tripoli baaada ya kuwasili kwa Waziri Mkuu Fayez Seraj pamoja na mafaasa wengine wa serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa.

Waziri huyo Mkuu wa Libya amekaribishwa na milio ya risasi, huku msafara wake ukikumbana na upinzani mkali kutoka kundi lililojitangazia madaraka linalodhibiti mji wa Tripoli likikidai kuja kwao ni jaribio la mapinduzi.

Serikali isiyotanbuliwa na jumuiya ya kimataifa katika mji mkuu wa Tripoli imekua ikibaini kwamba mipango inayofanywa na baraza la rais ni jaribio la mapinduzi. Baadhi ya mawaziri na maafisa wengine wa serikali hiyo wamesema watu hao wakamatwe.

Kituo cha televisheni cha libya Al Naab kimeshambuliwa na watu wenye silaha. Mpaka sasa kituo hicho kimefungwa na kimezuia kutangaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault amewasihi wananchi wa Libya kuwa na umoja na kudumisha amani kwa maslahi ya taifa lao.

"Nchi zote katika ukanda huo wanatarajia hali mpya ya kisiasa nchini Libya kwa sababu ni suala muhimu, ni suala la usalama, vinginevyo kundi la Islamic State linaendelea kujidhatiti," Bw Ayrault amesema.