Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mahakama ya kimataifa ya ICC kufuta kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto, Ziara ya rais wa Tanzania Magufuli nchini Rwanda

Sauti 21:07

Katika makala hii utasikia hatua ya mahakama ya kimtaifa ya ICC ya kuifuta kesi iliyokuwa inamkabili naibu rais wa Kenya William Ruto na mwanahabari Joshua Arap Sang kufwatia tuhma za kupanga na kochochea machafuko ya baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2007.Naibu rais wa Kenya William Ruto alisema kesi dhidi yake na Sang imesitishwa kwa sababu hawakuwa na kosa lolote.Wiki hii wananchi wa Rwanda walizindua wiki ya maombolezo katika muktadha wa maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini humo, ambapo mgeni wa heshima kutoka nje ya nchi alikuwa ni rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. ambaye pamoja na mwenyeji wake walizindua daraja la Rusumo mpakani mwa nchi hizo mbili.Huko DRC wiki hii umoja wa africa AU ulimteua waziri mkuu wa zamani Edem Kojo kuwa msuluhishi kwenye mazungumzo ya kitaifa nchini DRC.ungana nami Reuben Lukumbuka kusikiliza makala hii.