Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Sudan Kusini kusaini uanachama rasmi wa EAC, Mazungumzo ya kitaifa kuanza DRC na siasa za Brazil wiki hii.

Imechapishwa:

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesaini mkataba wa kuiingiza rasmi nchi yake hiyo kwenye Jumuiya ya Afrika mashariki jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo.Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.Sudan Kusini ni nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo, EAC.Nchini DRC mratibu wa mazungumzo ya kitaifa chini ya Umoja wa Afrika Edem Kodjo, anasema suala la kuheshimiwa kwa katiba ya nchi ndio linaonekana kuwa tatizo kubwa la sintofahamu ya kisiasa kuelekea uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Mazungumzo kujaribu kumaliza vita vilivyodumu kwa miaka mitano5 hivi sasa nchini Syria, yameng'oa nanga mjini Geneva,juma hili huku kukiwa na dalili zakutokea machafuko.

Sayari ya dunia
Sayari ya dunia
Vipindi vingine