COTE D'IVOIRE-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Namba 2 anaeshtumiwa mashambulizi ya Grand-Bassam akamatwa Mali

Askari wa Côte d’Ivoire katika eneo la mapumziko la Grand-Bassam, Machi 13, 2016, siku ya mashambulizi ya kigaidi.
Askari wa Côte d’Ivoire katika eneo la mapumziko la Grand-Bassam, Machi 13, 2016, siku ya mashambulizi ya kigaidi. © REUTERS/Luc Gnago

Moja wa washukiwa wakuu wa maandalizi ya mashambulizi ya eneo la mapumziko la Grand-Bassam, nchini Côte d’Ivoire amekamatwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mjini Bamako, nchini Mali, kulingana na taarifa zetu.

Matangazo ya kibiashara

Mtu huyu kutoka Mali alikuwa katika nafasi ya pili kwenye orodha ya watu wanaotafutwa baada ya mashambulizi ya Machi 13.

Alou Doumbouya, almaarufu "man" ni jina la mtu aliekamatwa. Alikuwa akifuatiliwa kwa siku kadhaa na vikosi maalumu vya Idara za Ujasusi za Mali ambazo zimeendesha operesheni ya kumkamata.

Chanzo kilio karibu na kesi hii kinaeleza kwamba ni namba mbili muhimu katika maandalizi ya mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya eneo la mapumziko la Grand-Bassam nchini Côte d’Ivoire.

Alou Doumbouya, raia wa Mali mwenye umri wa miaka 32 ameonyeshwa kama mtu aliesafirisha kutoka Mali kwenda Côte d’Ivoire, silaha zilizotumiwa katika mashambulizi dhidi ya eneo la mapumziko la Grand-Bassam. Alitumia moja ya matanki mawili ya mafuta ya gari lake la 4X4 kwa kuhifadhi silaha na risasi. Alou Doumbouya aliendesha mwenyewe gari hilo kutoka Mali hadi nchini Côte d’Ivoire, akiwasafuirisha watua walioendesha shambulizi hilo.