Pata taarifa kuu
LIBYA-MISRI-MAUAJI

Wahamiaji wengi kutoka Misri wauawa Libya

Martin Kobler katika mkutano na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Mitiga, Libya, Januari 1, 2016.
Martin Kobler katika mkutano na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Mitiga, Libya, Januari 1, 2016. REUTERS/Ismail Zitouny
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Wahamiaji kati ya kumi na mbili na kumi na sita kutoka Misri waliokua wakijaribu kuelekea Ulaya wameuawa katika makabiliano na wapita njia nchini Libya, Wizara ya mambo ya Nje ya Misri imetangaza Jumatano hii, Aprili 27, 2016.

Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na taarifa zetu za awali, wahamiaji haramu kati ya 12 na 16 kutoka Misri waliuawa katika mapigano na kundi la wapita njia," wizara imesema.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imebaini kwamba tukio hilo limetokea katika mji wa Bani Walid, sehemu wanakopitia wahamiaji, kwenye umbali wa kilomita 150 Kusini-Mashariki mwa mji wa Tripoli.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) kwa upande wake, umesema kuwa watu 15 ikiwa ni pamoja na raia 12 wa Misri na Walibya watatu wameuawa.

Katika taarifa yake, mkuu wa UJumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) Martin Kobler ameelezea masikitiko yake kufuatia mauaji hayo. Ametoa wito kwa serikali "kuhakikisha kwamba uchunguzi umefanyika na kuzuia mauaji zaidi kutokea nchini humo."

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.