Kiongozi wa waasi nchini Sudan kusini Riek Machar kurejea nchini, maadhimisho ya miaka 52 ya muungano nchini Tanzania

Sauti 20:05
Sayari ya dunia
Sayari ya dunia

Mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii tunaangazia mengi, ikiwemo Sudan kusini, ambako baada ya siku kadhaa za kuchelewa kurejea mjini Juba, nchini humo, hatimaye kiongozi wa waasi Riek Machar amewasili katika mji huo Jumanne Aprili 26.Tumeangazia pia maadhimisho ya miaka 52 ya muungano ya Tanzania, wakati huko Kenya, kifo cha mke wa rais wa zamani Mwai Kibaki, Bi Lucy Kibaki, na huko DRC mwili wa nguli wa miondoko ya rumba Papa Wemba kuwasili Kinshasa.Huko Marekani joto la uchaguzi kuzidi kupanda, lakini pia mapigano kule Syria.Ungana na mwandishi wetu Sabina Nabigambo kusikiliza zaidi.