LIBYA-WAHAMIAJI

Wahamiaji 15 watoweka katika bahari ya Mediterranean

Boti la wahamiaji likiondoka katika pwani ya Libya Mei 5, 2015.
Boti la wahamiaji likiondoka katika pwani ya Libya Mei 5, 2015. REUTERS/Ismail Zitouny

Ajali ya boti lililozama maji katika pwani ya Libya iligharimu maisha ya watu 15 siku ya Ijumaa, na kupelekea jumla ya idadi ya watu 100 waliokufa maji baada ya ajali nyingine ya boti kutokea siku hiyo hiyo, msemaji wa UNHCR amesema Jumapili hii.

Matangazo ya kibiashara

Inaarifiwa kuwa boti hilo lilikua lilibeba watu 120 wakati lilipozama siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya kuondoka katika pwani ya Libya, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Italia, Carlotta Sami, ameliambia shirika la habari la AFP, huku akiongeza kuwa watu 15 walikosekana.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Jumamosi, lilitoa idadi ya watu 84 walitoweka baada ya boti waliokuwemo kuzama, vile vile Ijumaa katika pwani ya Libya.

Ajali kama hizo zimekua zikitokea katika pwani ya Libya, na mpaka sasa maelfu ya wahamiaji wamepoteza maisha katika bahari ya Mediterranean wakijaribu kuingia Ulya kutafuta maisha. Jumuiya ya kimataifa imekua ikijitahidi kuzuia wimbi la wahamiaji wanaoondoka katika nchi zao na kukimbialia Ulaya kutafuta maisha bila mafaanikio. Wahamiaji wameendelea kukumbwa na masaibu mengi katika safari zao hizo hatari. Wengi wamekua wakisafiri usiku na kupita sehemu za kutisha.