RSF-Uhuru wa habari

Uhuru wa habari: Eritrea yachukua nafasi ya mwisho

Mwandishi wa habari wa Eritrea Dawit Isaak, mwenye asili ya Sweden, alikamatwa mwezi Septemba 2001 miongoni mwa waandishi wengine wanaotuhumiwa kuwa wapelelezi wa Ethiopia. Bado anashikiliwa Eritrea.
Mwandishi wa habari wa Eritrea Dawit Isaak, mwenye asili ya Sweden, alikamatwa mwezi Septemba 2001 miongoni mwa waandishi wengine wanaotuhumiwa kuwa wapelelezi wa Ethiopia. Bado anashikiliwa Eritrea. © AFP / Olivier Morin

Jumanne hii, Mei 3, inaadhimishwa siku ya kimataifa ya uhuru wa vyomvo vya habari. Barani Afrika, hali bado ni nzito hasa nchini Eritrea, ambayo imewekwa na shirika la Wanahabri Wasio na Mipaka (RSF) kwenye nafasi ya mwisho katika uhuru wa vyombo vya habari, huku Namibia ikiwekwa kati ya Canada na Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2007, Eritrea inashikilia nafasi ya mwisho (ya 180) katika orodhi hii iliyotolewa na cheo hiki kwa Wanahabari Wasiokuwa na Mipaka (RSF).

► Hali inayojiri Eritrea

Hatima wanahabari 11 wa Eritrea waliozuiliwa mwishoni mwa mwezi Septemba 2001, wakati huo dunia yote imekua ikiangazia tu macho nchini Marekani baada ya kukumbwa na mashambulizi, wiki moja kabla ya wanahabari hao kuwekwa kizuizini.

Wakati huo, Eritrea iliku huru ikiwa na magazeti yasiyozidi saba yaliyokua yakichapishwa katika mji mkuu, lakini wimbi la maandamano ndani ya serikali lilitokana na ukosefu wa uhuru.

Kwa mujibu wa askari wa zamani wa magereza, wafungwa wanne tu walinusurika hali ngumu ya kuzuiliwa katika la Eiraeiro, katika milima ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ambapo wanazuiliwa tangu wakati huo. Hata hivyo, hali yao ya kimwili na kiakili haijulikani.

Hii ndio sababu ilipelekea Eritrea kuwekwa kwenye nafasi ya mwisho katika uhuru wa vyombo vya habari duniani. Nchi hii pia imepewa nafasi hii ya fedheha mwaka huu wakati ambapo kuna taarifa zinazosema kuwa visa vya kujiua au ukosefu wa huduma, vimekithiri katika jela mbalimbali nchini humo.

Tangu mwaka 2001, hakuna mtu ambaye alikua na haki ya kutembelea wafungwa ikiwa ni pamoja na wanahabari hao, au kupata barua au kuonana na wanasheria wao. Hakuna kesi ambayo imekwishasikilizwa, wanapoulizwa viongozi wa Eritrea kuhusu watu hao,wanajibu kuwa hakuna mwaandishi wa habari anayezuiliwa.

"Nadhani kwamba kama kuna changamoto kubwa kwa miaka ijayo katika bara la Afrika ni kujumlisha sheria kwa kupata ambazo zitapelekea waandishi wa habari kufanya kazi yao vizuri zaidi katika mazingira mazuri ya usalama kwa sababu kwa kupata habari za kuaminika ndio sababu wabakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwekwa jela, " Clea Kahn-Sriber, kiongozi wa RSF katika Ukanda wa Afrika amesema.

► Burundi "yaandelea kujichimbia shimo"

Barani Afrika, Burundi imepoteza nafasi 11 na sasa inachukua nafasi ya 156 kwa sababu "vitendo vya ukatili dhidi ya wanahabri vilishuhudiwa katika nchi hii baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kugombea muhula tata wa tatu, " RSF imeandika.