MISRI-WANAHABARI

Mvutano kati ya chama cha wanahabari na Wizara ya Mambo ya Ndani

Aprili 28, waandishi wa habari wameandamana nje ya makao makuu ya cham cha waandishi wa habari dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri.
Aprili 28, waandishi wa habari wameandamana nje ya makao makuu ya cham cha waandishi wa habari dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany

Nchini Misri, chama cha waandishi wa habari kilifanyika mkutano maalum Jumatano hii, Mei 4 na kuhudhuriwa na maelfu ya waandishi wa habari licha ya vizuizi vya barabarani vilivyowekwa na polisi na mashambulizi ya baadhi ya wanahabari.

Matangazo ya kibiashara

Chama, ambacho kinawakilisha magazeti, kimepitisha mfululizo wa hatua zinazomlenga hasa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mvutano kati ya serikali na waandishi wa habari unaendelea. Waziri wa Mambo wa Mambo ya Ndani Magdy Abdel Ghaffar hataki "mtu" yeyote kuweka picha yake kwenye kurasa za magazeti. Waziri ambaye kuachishwa kwake kazi ni sharti muhimu kwa ajili ya kutatua mgogoro.

Zaidi ya nusu ya wajumbe wa chama waandishi wa habari walihudhuria mkutano huo. Mkutano hu ulifanyika katika hali ya sintofahamu: "Uhuru katika taifa huru. Misri juu zaidi na uhuru wa habari pamoja na umoja wa waandishi wa habari juu zaidi, " Yehia Qalash, kiongozi wa chama cha wanahabari ameaakisem akatika ufunguzi wa hotuba yake.

"Kususia vyombo vya habari vyenye udhaifu"

Waandishi wa habari pia wameamua kuchapisha nembo kwenye magazeti yote dhidi ya "marufuku ya kuchapisha." Mwendesha mashitaka mkuu amepiga marufuku ya kuchapisha habari yoyote kuhusu uvamizi wa polisi dhidi ya makao makuu ya chama cha waandishi wa habari, Jumapili, Mei 1.

Wizara ya mambo ya Ndani pia imemtishia kiongozi wa chama cha waandishi wa habari kuwa utamfungulia mashtaka. Wakati huo huo, harakati zimeanzishwa katika vyombo vya habari vinavyorusha habari zao kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kauli mbiu "Kususia vyombo vya habari dhaifu" kwa kusikiliza "vile muhimu vyenye uzoefu katika taaluma ya uandishi".