Karibu katika makala ya habari rafiki hii leo tutajadili kuhusu suala la maadili katika kazi za sanaa hususani katika sanaa ya muziki,filamu na zinazofanana na hizo ndani ya jamii Afrika mashariki na kati.Kwa kiasi gani maadili yanasimamiwa ili kutoipotosha jamii? Juma hili Baraza la sanaa nchini Tanzania lilipiga marufuku kuoneshwa kwa video ya wimbo Chura wa msanii Snura kwa madai kuwa video hiyo ilikosa maadili na hivyo kama ingeoneshwa ingeleta picha mbaya kwa jamii.Marufuku hii ilishawahi kufanywa pia nchini Kenya kwa kundi la Saut Sol na wimbo wao wa Nishike hali kadhalika pia nchini Uganda wasanii kadhaa nyimbo zao zilipigwa marufuku kuoneshwa kwenye televisheni.Msikilizaji una mchango gani katika hili? Je ni kweli wasanii wanapenda kuiga vitu vya nje zaidi kuliko kuzingatia mandhari ya afrika ambako nyimbo zao huoneshwa?