Mali: kiongozi mkuu wa kijihadi akamatwa

Militaire malien en patrouille.
Militaire malien en patrouille. © AFP PHOTO / KAMBOU SIA

Mtu anayetuhumiwa kuwa kiongozi namba mbili wa Ansar Dine, moja ya makundi ya kijihadi nchini Mali, amekamatwa karibu na mji wa Bamako. Mtu huyo anatuhumiwa kuwapa silaha wapiganaji wa kijihadi kwa lengo la kushambulia kusini mwa Mali na nchi jirani ya Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Yacouba Touré, mwenye umri wa miaka 40, raia wa Mali, amekamatwa na vikosi vya Idara ya Ujasusi nchini Mali. Ameonyeshwa kama namba mbili wa kundi la Ansar Dine Kusini mwa Mali.

Kundi hili, ambalo linaendesha operesheni kusini mwa Mali ni kitengo kikuu cha kundi jingine la Kiislam kaskazini mwa Mali, linalojulikana kwa jina la Ansar Dine na linaongozwa na Iyad Ag Ghaly, kutoka mkoa wa Kidal.

Pamoja mwili wake wa bondia, Yacouba Touré pia amekua akiwapa silaha wanajihadi kusini mwa Mali, chanzo kilio karibu na uchunguzi kimesema. Kwa mujibu wa chanzo hicho, pia Yacouba Toure amekua akitoa silaha kwa tawi changa la kundi la Ansar Dine nchini Burkina Faso.

Maelezo: Katika kauli yake ya kwanza kwa wachunguzi, Yacouba Touré alisema kuwa mwaka 2010 alikuwa katika safu ya wanamgambo wa Kiislam kaskazini mwa Mali ambako alimtambua Boubacar Sawadogo, raia wa Burkina Faso. mtu huyo kwa sasa anaongoza kitengo maalumu kinachohusika na kutekeleza mashambulizi nchini Burkina Faso.

Tarehe 9 Oktoba 2015, Boubacar Sawadogo na watu wake, baada ya kupewa silaha na Yacouba Touré, walishambuliwa kituo cha polisi cha Samorogouan nchini Burkina Faso, na kuua askari polisi.