DRC-KATUMBI-SIASA

Eric Dupond-Moretti mwanasheria mpya wa Moïse Katumbi

Wakili Eric Dupond-Moretti, mwanasheria wa masuala ya jinai kutoka Ufaransa, amekubali kumsaidia mpinzani wa DR Congo Moïse Katumbi katika utetezi wake.

Mwanasheria wa masuala ya jinai kutoka Ufaransa, Eric Dupont-Moretti, amekubali kumtetea mpinzani wa DR Congo Moise Katumbi, Mei 10, 2016.
Mwanasheria wa masuala ya jinai kutoka Ufaransa, Eric Dupont-Moretti, amekubali kumtetea mpinzani wa DR Congo Moise Katumbi, Mei 10, 2016. © AFP/MEHDI FEDOUACH
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga na mgombea urais anatuhumiwa na mahakama ya nchi hiyo "kuajiri askari mamluki", hasa Wamarekani.

Moïse Katumbi atasikilizwa tena Jumatano na mwendesha mashtaka mjini Lubumbashi katika mfumo wa uchunguzi kuhusu madai ya kuajiri askari mamluki wa kigeni. Baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba Jumatatu wiki hii, Moïse Katumbi ameamua kuimarisha utetezi wake katika siku moja kabla ya kusikilizwa tena, kwa kumshirikisha katika timu yake ya wanasheria wa Congo mwanasheria mashuhuri wa chama cha mawakili wa Ufaransa: Wakili Eric Dupond-Moretti.

"Mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yanasema kuwa kesi ni haieleweki, kesi ya kisiasa yenye lengo tu kumzuia Moïse Katumbi kutowania katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwaka huu, " Bw Eric Dupond-Moretti ameiambia RFI. Ameongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa "kusafirishwa mjini Kinshasa" kwa mwanasiasa huyo wa upinzani wa Congo. "

Wiki iliyopita, Moïse Katumbi alitangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika mwaka huu. Aliposikilizwa kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii, Bw Katumbi alikana tuhuma dhidi yake.