Moïse Katumbi kusikilizwa kwa mara nyingine na Mwendesha mashitaka
Imechapishwa: Imehaririwa:
Moïse Katumbi anatazamiwa kusikilizwa tena leo Jumatano na Mwendesha mashtaka mjini Lubumbashi katika mfumo wa uchunguzi kuhusu madai ya kuajiri askari mamluki wa kigeni.
Baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba Jumatatu wiki hii, Moïse Katumbi ameamua kuimarisha utetezi wake, kwa kumshirikisha katika timu yake ya wanasheria wa Congo mwanasheria mashuhuri wa chama cha mawakili nchini Ufaransa: Wakili Eric Dupond-Moretti.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga na mgombea urais anatuhumiwa na mahakama ya nchi hiyo "kuajiri askari mamluki", hasa Wamarekani.
"Mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yanasema kuwa kesi hii haieleweki, na kesi ya kisiasa yenye lengo tu kumzuia Moïse Katumbi kutowania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka huu, " Bw Eric Dupond-Moretti ameiambia RFI. Ameongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa "kusamfirisha mjini Kinshasa" mwanasiasa huyo wa upinzani wa Congo.
Wiki iliyopita, Moïse Katumbi alitangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika mwaka huu. Aliposikilizwa kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii, Bw Katumbi alikana tuhuma dhidi yake.
Jumapili hii, Moïse Katumbi, kwenye akaunti yake ya twitter, ameiomba serikali iwajibike kwa usalama wa raia wa Jmhuri ya Kidemokrasia ya Congo badala ya kubuni kesi za uzushi dhidi yake.
"Serikali yetu inapaswa kuchukua hatua kuanzia sasa: kuongezeka juhudi za kijeshi, polisi na kisheria kwa kuhakikisha usalama umerejea nchini. Badala kubuni kesi bandia katika mji wa Lubumbashi, " amesema Bw Katumbi, huku akiwapongeza raia kumuunga mkono wakati alipokua akisikilizwa katika ofisi ya mashitaka mjini Lubumbashi Jumatatu wiki hii.
3/ Notre gouvernement doit maintenant agir: accroissement des efforts militaires, policiers, juridiques. Au lieu des faux procès à L'shi.
— Moise Katumbi (@moise_katumbi) May 9, 2016
1/ Merci à la population venue si nombreuse réclamer une justice équitable. Votre soutien me renforce dans ma lutte. L'Etat de droit vaincra
— Moise Katumbi (@moise_katumbi) May 9, 2016