TUNISIA-USALAMA
Polisi 4 na washukiwa 3 wa kijihadi wauawa Tunisia
Imechapishwa:
Polisi wanne na washukiwa watatu wa Kijihadi wameuawa baada ya operesheni ya kiusalama Kusini mwa nchi ya Tunisia.
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya Mambo ya ndani inasema mauaji hayo yalitokana baada ya makabiliano makali kati ya polisi na wanajihadi hao.
Mbali na hilo, watu wengine kumi na sita walikamatwa katika mji wa Ariana wakiwa wamejihami kwa silaha.
Wanajihadi na maafisa wa polisi wamekuwa wakikabiliana na maafisa wa usalama tangu mwaka 2011 baada ya mapinduzi dhidi ya serikali iliyopita.