KOREA KASKAZINI DRC

Korea kaskazini yasambaza bastola DRC

Wanajeshi wa jeshi la DRC wanatajwa kusambaziwa bastola na Korea Kaskazini
Wanajeshi wa jeshi la DRC wanatajwa kusambaziwa bastola na Korea Kaskazini Reuters

Korea kaskazini imeripotiwa kusambaza bastola nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo,silaha ambazo huishia mikononi mwa walinda amani wa taifa la jamuhuri ya afrika ya kati,kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa UN.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti iliyoonwa na AFP Jopo la wataalamu liligundua bastola hizo kuwa na alama sawa na zinazotengenezwa na Korea kaskazini na kuonekana kwa maafisa fulani wa jeshi la FRDC na polisi wa Congo ambao wanahudumu katika jeshi la umoja wa mataifa jamuhuri ya afrika ya kati MINUSCA.

Korea kaskazini ilipigwa marufuku kuuza silaha na kununua, au pia kutoa mafunzo wakati marufuku dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo iliitaka nchi hiyo kuiarifu kamati ya vikwazo katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa juu ya biashara yoyote ya kununua au kupokea mafunzo.

Wataalamu hao wanasema wamegundua kuwa maafisa kadhaa wa jeshi la Congo pamoja na maafisa wa polisi  wa Umoja wa Mataifa, wanaonekana kuwa na bastola hizo za Korea Kaskazini.