LIBYA-IS

Askari polisi zaidi ya 30 wa serikali ya Tripoli wauawa

Askari polisi 32 wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya wameuawa Jumatano Mei 18 katika shambulio la kujitoa mhanga kwa bomu lililotegwa ndani ya gari na katika mapigano na kundi la Islamic State kilomita 60 magharibi mwa mji wa Sirte, ngome ya wapiganaji wa kijihadi nchini humo.

Majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya katika mji wa Abu Grein, baada ya kutangazwa udhibiti wa mji huo.
Majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya katika mji wa Abu Grein, baada ya kutangazwa udhibiti wa mji huo. © MISRATA TV via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yalizuka karibu na mji wa Abu Grein, ulio kwenye umbali wa kilomita 130 magharibi mwa mji wa Sirte nakudhibitiwa Jumanne na vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli kutoka mikononi mwa kundi la Islamic State.

Mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari ulitokea katika kijiji cha El-Hassoun Bouairat kilomita 60 magharibi mwa mji wa Sirte, ngome ya kundil a Islamic State nchini Libya. Lakini majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa yanadai kuwa yamefaulu kudhibiti kijiji hiki.

Kwa jumla askari polisi thelathini na mbili wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya waliuawa Jumatano wiki hii, kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni kutoka kituo cha operesheni za kijeshi.

Mapigano ya kurejesha maeneo yanayoshikiliwa na kundi la IS

Majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa na yale ya serikali hasimu yenye mako yake mashariki mwa kila upande umeanzisha katika mashindano ya kuwa wa kwanza mashambulizi kabambe yenye lengo la kulitimua kundi la wanajihad wa Islamic State na kudhibiti ngome yao ya Sirte kilomita 400 mashariki mwa mji wa Tripoli. Shindano hili linaangaliwa kwa shingo la upande na jumuiya ya kimataifa ambayo inabaini kwamba huenda likahatarisha juhudi za kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali nchini Libya.

Siku ya Jumatano, shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Human Rights Watch lililituhumu kundi la wanajihadi kuwa liliendesha visa 49 vya mauaji kwa watu ambao lilikua limewashikilia katika mji wa Sirte na kuwaweka hatarini wakazi wa mji huu wa mwambao katika "maisha magumu", na hivyo kuwaibia chakula, dawa, mafuta na fedha. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo, zaidi ya theluthi mbili ya wakazi 80 000 wa mji huo walikimbia baada ya kuwasili kwa kundi la IS mwishoni mwa mwaka 2014.