DRC-KATUMBI-SIASA

DRC: Moïse Katumbi ashtakiwa kwa kosa la "kuajiri mamluki "

Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016.
Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016. © REUTERS/Kenny Katombe

Mwanasiasa wa upinzani Moïse Katumbi, mgombea aliyejitangaza kuwania kiti cha urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ameshtakiwa Alhamisi hii Mei 19 kwa kosa la "kuhatarisha usalama wa ndani na nje ya nchi", Mwendesha mashtaka mkuu wa Jamhuri mjini Kinshasa amesema.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mashtaka yanakwenda sambamba na mwisho wa hatua ya uchunguzi na mkuu wa zamani wa zamani wa mkoa wa Katanga sasa anasubiri rasmi kesi kuanza.

Moïse Katumbi anashtumiwa na serikali ya Congo kuajiri mamluki kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa, wiki kadhaa baada ya kuchukua uamuzi wa kurasimisha kugombea kwake katika kiti cha urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka huu.

Jumatano Mei 4 Waziri wa sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, Alexis Thambwe Mwamba alisema kwamba aliamuru uchunguzi kuhusu madai ya "kuajiriwa kwa mamluki" wa kigeni yanayohusishwa mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga (kusini), Moïse Katumbi.

"Ninatoa amri kwa PGR (Mwendesha mashitaka mkuu wa Jamhuri) kuanzisha uchunguzi katika mkoa wa zamani wa Katanga (...) Tuna nyaraka za ushahidi kuwa askari kadhaa wa zamani wa Marekani ambao kwa sasa wako Katanga wanafanya kazi kwa maslahi ya Bw. Katumbi , " Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Alexis Thambwe Mwamba, alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

"Mtego wa ujanja tena hatari"

"Utawala unataka kunidhuru na mambo yote yako sawa. Nina imani na raia na waangalizi wa kimataifa ambao hawaanguka katika mtego huu wa ujanja na hatari ", Moïse Katumbi alitangaza wiki mbili zilizopita.

Katumbi mwenye umri wa miaka 51 alijiunga na upinzani mwezi Septemba, baada ya kujiuzulu kama mkuu wa mkoa wa Katanga (kusini)na aliondoka katika chama cha urais. Bw Katumbi ni mmoja wawatu maarufu nchini Congo, mfanyabiashara tajiri pia ni kiongozi wa kifahari wa klabu ya soka ya Tout-Puissant Mazembe ya Lubumbashi, mshindi mara tatu wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Hali ya kisiasa imeendelea kuwa tete kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa uwezekano mkubwa wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba. Upinzani anamtuhumu Kabila, madarakani tangu mwaka 2001 na ambaye Katiba inampiga marufuku ya kuwania katika uchaguzi huo.

Wafuasi wa Moïse Katumbi mbele ya mahakama Mei 11, 2016.
Wafuasi wa Moïse Katumbi mbele ya mahakama Mei 11, 2016. REUTERS/Kenny Katombe