DRC-BENI-USALAMA

FARDC na MONUSCO waendesha operesheni Beni

Kamanda wa Jeshi la MONUSCO (kulia) amemtembelea katika majukumu ya kazi, Jumanne, Aprili 5, 2016, kamanda wa operesheni Sokola katika wilaya ya Beni akiwepo jenerali Mushale (kushoto), mkku wa kanda ya 3 ya kijeshi DRC.
Kamanda wa Jeshi la MONUSCO (kulia) amemtembelea katika majukumu ya kazi, Jumanne, Aprili 5, 2016, kamanda wa operesheni Sokola katika wilaya ya Beni akiwepo jenerali Mushale (kushoto), mkku wa kanda ya 3 ya kijeshi DRC. © Photo MONUSCO/Force

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu Wilaya ya Beni inakabiliwa na mauaji yanayohusishwa kundi la waasi wa Uganda la ADF licha operesheni ya mara kwa mara ya jeshi la Congo au hata operesheni za kikosi cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO).

Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumatano wiki hii, vyama vya kiraia wilayani Beni vimetangaza siku tatu za kususia kazi. Katika mkoa wa Kivu ya Kusini, vyama hivyo vya kiraia vinajiandaa kwa ajili ya maombolezo siku ya Ijumaa nakuwatolea wito raia kuvaa nguo nyeusi.

Wakati huo huo, jeshi la Congo na kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO) wametangaza kwamba tayari wameanzisha operesheni mpya ya pamoja tangu Jumamosi iliyopita, operesheni ijulikanayo kwa jina la Usalama.

Tangu kushindwa kwa kundi la waasi wa zamani la M23, kulikuwa na kiwango hicho cha ushirikiano, jeshi la Congo (FARDC) na MONUSCO wamethibitisha. Hakuna mabadiliko katika makao makuu ya jeshi la Congo katika wilaya ya Beni, lakini wanajeshi watakua wakibadilishwa mara kwa mar, upande wa jeshi wamebaini. Upande wa MONUSCO, ndege zisio narubani, helikopta, vikosi maalum na askari wapya na vifaa muhimu vinatumiwa katika operesheni hiyo. "Kuna ulazima wa kutambua kwamba kuna sehemu ya wajibu wa kila mmoja wa kutozuia mauaji haya," Umoja wa Mataifa umekiri.

Vikosi hivi viwili vya majeshi vimehakikisha kwamba tayari kuna matokeo mazuri: baadhi ya wapiganaji wa kundi la waasi la ADF wameuawa, kuna baadhi ya ngome za waasi hao ambazo ziliteketezwa na kudhibitiwa bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi kwa sasa. Jeshi la Congo ndio lina haki ya mawasiliano, moja ya masharti yaliyowekwa na serikali ya Kinshasa kabla ya kuanza ushirikiano huo. Lakini mtaalam wa Congo, Jason Stearns, amesema ili operesheni hiyo ifaulu, inabidi kumtambua kwanza adui.

Hata hivyo, ripoti mbili zimetofautiana na toleo rasmi la jeshi la Congo (FARDC na kikosi cha MONUSCO na kudai kwamba wanamgambo na hata wanajeshi wa Congo huenda wamehusika katika mauaji hayo. Mtaalam huyo amependekeza uchunguzi wa kina kuhusu mauaji hayo ufanyike.