MISRI-EGYPTAIR

Misri bado yajiuliza chanzo cha ajali ya ndege ya EgyptAir

Familia ya abiria waliosafiri katika yeneye chapa MS804 wakiwasili kwa basi katika uwanja wa ndege wa Cairo Mei 19, 2016.
Familia ya abiria waliosafiri katika yeneye chapa MS804 wakiwasili kwa basi katika uwanja wa ndege wa Cairo Mei 19, 2016. AFP

Waziri wa Usafiri wa Anga wa Misri amesema Alhamisi hii kuwa nchi yake haijajua kile ambacho kimesababisha ajali ya ndege ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir iliyokua ikitokea Paris ikielekea Cairo.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hii ilitoweka mapema Alhamisi hii asubuhi katika eneo la bahari ya Mediterranean baada ya kutoweka kwenye mitambo ya rada. Mpaka sasa mamlaka ya Misri haijafahamu iwapo ajali ya ndege hiyo imesababishwa na tatizo la kiufundi au kitendo cha kigaidi.

"Endapo mtu anauliza kama ndege hiyo imeanguka au ajali ya ndege hiyo imesababishwa na nini, nitakosa la kumjibu," Waziri Sherif Fathy amesema akiwaambia waandishi wa habari. "Siwezi kukataa Dhana ya kitendo cha kigaidi, au kitu ambacho ikimetokea kama tatizo la kiufundi, ni mapema mno," bw Fathy ameongeza.

Kwa mujibu wa mamlaka ya usafiri wa anga ya Ugiriki na Rais wa Ufaransa Francois Hollande ndege ya shirika la ndege la EgyptAir ilianguka katika bahari ya Mediterranean ikiwa na watu 66.

Hata hivyo jeshi la Ugiriki limebaini kwamba mabaki yanayokisiwa kuwa ya ndege ya shirika la ndege la EgyptAir iliyotoweka mapema asubuhi, yamegunduliwa katika pwani ya kisiwa cha Ugiriki.

"Baadhi ya vifaa vya ndege ya EgyptAir vimegunduliwa kusini mashariki mwa katika eneo la anga linalomilikiwa na Misri. Meli zimetumwa katika eneo hilo, " msemaji wa jeshi la Ugiriki, Vassilis Baletsiotis amesema.