NIGERIA-BOKO HARAM-CHIBOK

Nigeria: Msichana wa pili mwanafunzi wa Chibok apatikana

Maandamano ya familia ya wasichana wa shul ya sekondari ya Chibok, Alhamisi, 27 Agosti  Abuja.
Maandamano ya familia ya wasichana wa shul ya sekondari ya Chibok, Alhamisi, 27 Agosti Abuja. © REUTERS/Afolabi Sotunde

Jeshi la Nigeria limetangaza Alhamisi hii Mei 19 kuwa limemuokoa msichana wa pili miongoni mwa wanafunzi 219 wa shule ya sekondari ya Chibok waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram mwaka 2014, saa chache baada ya Rais Buhari kukutana kwa mazungumzo na Amina Ali.

Matangazo ya kibiashara

Amina Ali ni mwanafunzi wa kwanza wa shule ya sekondari ya Chibok aliyeokolewa Jumanne wiki hii.

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Nigeria, Kanali Sani Usman, mateka wa pili wa Chibok alikuwa miongoni mwa wanawake 97 na watoto waliookolewa Alhamisi wakati wa operesheni ya pamoja ya jeshi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali saa 5:00 mchana (sawa na saa 4:00 saa za kimataifa) karibu na mji wa Damboa katika jimbo la Borno, kaskazini mwa Nigeria.

"Jina lake ni Serah Luka, yuko kwenye namba 157 kwenye orodha ya wasichana waliotekwa nyara. Inadhaniwa ni binti wa Mchungaji Luka, " Kanali Usman ameongeza, huku akibaini kwamba msichana huyo amekua akipewa hudumaza kimatibabu katika kambi ya jeshi ya Biu, katika jimbo la Borno. Serah Luka, ni kutoka kijiji cha Madagali katika jimbo jirani la Adamawa, na alikua alijiunga na shule ya sekondari ya Chibok miezi miwili kabla ya kutekwa nyara, jeshi limebainisha.

Mapema Alhamisi wiki hii, Amina Ali, mateka wa kwanza wa shule ya sekondari ya Chibok aliyepatikana Jumanne wiki na walizi wa msitu kwa ushirikiano na jeshi, alisafirishwa Abuja kwa ndege kutoka Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, na mama yake, Binta, kukutana na Rais Muhammadu Buhari.

Baada ya kukutana kwa mazungumzo na msichana huyo, Bw Buhari alihakikisha kwamba "serikali itafanya kilio chini ya uwezo wake kwa kuwaokoa wasichana wengine wa shule ya Chibok". "Kuokolewa kwa Amina kunatufanya tuwe na matumaini mapya, na tumepata fursa ya kipekee katika suala la taarifa muhimu," Rais Buhari amesema.

Aprili 14, 2014, kundi la Boko Haram liliteka nyara wasichana 276 kutoka shule ya sekondari ya Chibok. Hamsini na saba kati yao walifanikiwa kutoroka katika masaa kadhaa baada ya kutekwa nyara na kundi la Boko Haram.