SUDAN-UN

Sudan haiko tayari UN kuongeza muda wa kikosi chake

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, Khartoum, Aprili 18, 2012
Rais wa Sudan Omar al-Bashir, Khartoum, Aprili 18, 2012 Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah

Sudan inasema haitaomba Jumuiya ya Kimataifa kuwaongezea muda zaidi vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyohudumu katika jimbo la Darfur baada ya muda wao kukamilika mwezi Juni.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje inasema hali ya utulivu imeshaanza kurejea katika jimbo hilo na raia wanasema wako salama na hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwepo kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana hivi karibuni kukubaliana kuwaongezea wanajeshi hao mwaka mmoja kuendelea kutathmini hali ya usalama katika jimbo hilo.